WALIMU BOKO TIMIZA WAKOMBOLEWA NA MAMA KOKA KWA VITI NA MEZA

NAVICTOR MASANGU, KIBAHA

Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka ametekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kukabidhi viti na meza kwa walimu wa shule ya msingi Boko Timiza iliyopo kata ya Tumbi Halmashauri ya Kibaha mjini waliokuwa wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa viti na meza kwa ajili ya kukalia katika ofisi yao.

Akikabidhi msaada huo wa viti kumi pamoja na meza zake Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini SaidMbecha kwa niaba ya mke wa Mbunge amesema kwamba Mama Koka ameamua kutekeleza ahadi yake kwa vitendo ambayo aliitoa wakati wa halfa ya mahafali ya kuhitimu wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo ya msingi Boko Timiza.

Mbecha alisema kwamba Mama Koka ametoa vifaa hivyo kutokana na kupokea risala kutoka kwa walimu hao ambayo ilikuwa inaeleza cahnagamoto mbali mbali walizonazo ikiwemo ya ukosefu wa viti na meza katika ofisi yao hivyo kupelekea kukaa katika mazingira magumu katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao ya kila sika katika kuwahudumia wanafunzi.

“Shule hii ya msingi Boko Timiza katika halfla ya kumaliza wanafunzi wa darasa la saba ambayo ilifanyika hivi karibuni walimu na wanafunzi walieleza chanagmoto zao mbali mbali na moja ikiwa ni ukosefu wa samani ya viti na meza hivyo kwa kuliona hilo Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka ametekeleza ahadi ambayo aliitoa na nimekuja kwa niaba yake kukabidhi viti na meza,”alibainisha Mbecha.

Kadhalika Mbecha alifafanua kwamba mbali na kukabidhi viti na meza ameweza kukabidhi sukari kilo kumi ambazo zitaweza kuwasaidia walimu waweze kupata chai nyakati za asubuhi ili waweze kufundisha walimu wakiwa katika hali nzuri lengo ikiwa ni kuweza kuongeza kasi ya ufundishaji na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Boko Timiza Rozania Kimate amemshukuru kwa dhati Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka kwa kuweza kutekeleza ahadi yake kwa vitendo ambayo aliitoa wakati mahafali ya darasa la saba ya kuwasaidia walimu hao viti na meza ili waondokana na changamoto ambayo walikuwa wanakabiliana nayo ya kukaa katika mazingira magumu.

Mwalimu huyo amebainisha kwamba katika shule hiyo hapo awali walikuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo hiyo ya viti na meza lakini kutokana na kuguswa ameweza kutekeleza ahadi hiyo ya viti na meza ikiwemo pamoja na sukari, bilika kwa ajili ya chai ambayo kwa upande wao ni msaada mkubwa sana katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku katika ufundishaji wa wanafunzi.

Naye Mwenyekiti kamati ya shule ya msingi Boko Timiza Michael Mwampashi hakusita kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka kwa juhudi zake za kushirikiana na wananchi wa Boko Timiza katika kuhakikisha anaboresha na kuweka mazingira mazuri ya kuisaidia kwa hali na mali yeye pamoja na mke wake Mama Selina Koka katika kusaidia mambo mbali mbali ikiwemo viti na meza.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Boko Temboni Said Mohamed amesema msaada huo ambao umetolewa na Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini wa viti na meza utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa walimu ambao hapo awali walikuwa na adha kubwa ya ofisi yao kukosa vifaa mbali mbali ikiwemo ukosefu wa samani ya viti na meza na kumshukuru Mbunge Koka kwa kushiriki katika juhudi za kuiboresha shule hiyo katika miundombinu ya majengo ya madarasa.

 

Related Posts