SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa) limempiga marufuku gwiji wa soka nchini Cameroon, Samuel Eto’o kuanzia Jumatatu hii kuhudhuria michezo yoyote ya timu ya taifa kwa miezi sita.
Eto’o, ambaye amekuwa rais wa shirikisho la soka la Cameroon tangu 2021, amekabiliwa na mashtaka mawili kutokana na tukio kwenye mashindano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 20 nchini Colombia mnamo 11 Septemba.
FIFA haikueleza undani wa kilichotokea katika mchezo wa hatua ya 16 bora ambao Brazil walishinda dhidi ya Cameroon 3-1 baada ya muda wa ziada.
Eto’o alihukumiwa kuwa alivunja sheria za kinidhamu zinazohusiana na “tabia ya kukera na ukiukaji wa kanuni za mchezo wa uungwana” na utovu wa nidhamu wa maafisa, FIFA imesema.