Jasmine Akabidhi Simu janja , kwaajili ya Uvccm Kukamilisha uchaguzi

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya ya Mufindi, Jasmine Ng’umbi, ametoa simu janja kwa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Iringa, akisisitiza kuwa zitatumika kuimarisha zoezi la usajili wa wanachama.

Pia, alikabidhi jora nane la vitambaa kwa ajili ya vijana wa Itifaki, ili waweze kushona sare, kutokana na mchango mkubwa wa vijana hao katika chama cha Mapinduzi.

Jasmine alitoa msaada huu wakati wa kufungwa kwa mafunzo maalum ya vijana wa CCM kutoka kata mbalimbali za Mkoa wa Iringa, yaliyofanyika katika Chuo cha Vijana Ihemi.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Salim Abri Asas.

Akizungumza katika hafla hiyo, Jasmine alisema mafunzo hayo yamekuwa na tija kubwa kwa vijana, kwani yameongeza ari ya kujenga chama chao, uvumilivu, na kuelewa sifa za uongozi.

Aliwashauri vijana kujiandaa kugombea nafasi mbalimbali na kuwa sehemu ya upatikanaji wa viongozi bora.


Wakati wa makabidhiano ya zawadi hizo, Asas aliwataka vijana kuendelea kujitolea ndani ya chama, huku akimpongeza Jasmine kwa juhudi zake katika shughuli za chama ambapo hivi karibuni alimteua Jasmine kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ujenzi wa Ofisi za Kata Wilaya ya Mufindi, hatua inayothibitisha dhamira yake ya kuleta mabadiliko chanya katika chama

Related Posts