Michezo kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi Mpimbwe

Mashabiki wa timu ya Simba na Yanga halmshauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wameoneshana ubabe katika tamasha maalum la kuhamasisha watu kushiriki zoezi.la kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kuanzia octoba 11 hadi 20 maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika novemba 27 mwaka huu

 

Akizungumza katika tamasha Hilo mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo Kavu Mhe Godfrey Pinda ambaye ni naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo amewataka wananchi kuhakikisha wnashiriki kwenye zoezi hilo Ili kupata viongozi Bora kwwmye vitongoji,mitaa na vitongoji vyao Kwa kipindi cha miaka mitano ijayo

 

Mhe. Pinda amesema huwezi kupata maendendeleo bila kuchagua kiongozi Bora ambao ndio msingi wa maendeleo hayo kuanzia ngazi ya kitingoji Hadi Taifa.

Anasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan anatoa pesa nyingi Kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo inahitajika viongozi wazaLendo wanaoweza kusimamia miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.

 

Tamasha hilo la mchezo wa hisani umeandaliwa na mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Mpimbwe Shamim Daudi Mwariko mkuu wa Wilaya hiyo ya Mlele Alhaj Majid Mwanga akihudhiria.

Zaidi watu 1500 Wapenzi wa Yanga na Simba walishiriki ktk mtanange huo ambapo mashambiki wa timu ya Simba wameshinda goli 3 na timu ya Yanga 2.

Lengo ni kuhamasisha wananchi kushiriki nzoezi la Uandikishaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa washidi walikipatia zawadi mbalimbali ikiweo mbuzi wa na fedha taslimu.

 

Aidha mechi hiyo ilitqnguliwa na Jogging asubuhi ,kufanya Usafi Maendeleo mbalimbali ya Halmashauri michezo kama ya kuvuta kamba kukimbia ktkagunia na kufuluza kuku na mwisho Gwaride maalumu la vijana wa wa Jeshi la akiba

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na vijiji hufanyika kila.baada ya miaka mitano ukishirikisha vyama mbalimbali vya siasa ambayo vimesajili kisheria.

Related Posts