Uamuzi juu ya dhamana ya Meya wa zamani, Boniface Jacob kutolewa Octoba 7 2024

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga October 7, 2024 kutoa uamuzi juu ya dhamana ya Meya wa zamani, Boniface Jacob baada ya hii leo kutupilia mbali maombi ya Serikali juu kiapo cha ziada katika kiapo cha awali.

Nje ya mahakama, Wakili wa utetezi Peter Kibatala amezungumza na vyombo vya habari kuhusu hoja za serikali zilizotupiliwa mbali sambamba na matarajio ya uamuzi wa October 7 utakaotolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Franco Kiswaga.

“Tunafurahi leo mahakama imekubali hoja zetu zote imetupilia mbati hoja za serikali kuna kipande kimebakia cha dhamana ambapo mahakama imepanga tarehe 7, 10,2024 kwa ajili ya uamuzi”

Jacob alifikishwa mahakamani, September 19, 2024 na kisha kuwekewa pingamizi la dhamana katika kesi inayomkabili ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.

Related Posts