UKUBWA wa timu ya Vijana Queens katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), ulionekana katika mchezo dhidi ya DB Troncatti baada ya kushinda kwa pointi 62-59, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Donbosco, Oysterbay.
Wengi wa watazamaji waliofurika katika uwanja huo waliamini Vijana Queens ingepoteza mchezo kutokana na kiwango cha chini ilichoonyesha katika robo mbili za kwanza.
Timu ya DB Troncatti ikimtumia Jesca Lenga ilionekana ni mwiba kwa walinzi wa Vijana Queens kutokana na asisti alizokuwa akitoa kwa wafungaji.
Jesca anayecheza nafasi ya kati (point guard) alichangia kwa kiasi kikubwa timu yake kuongoza katika robo mbili za kwanza kwa pointi 20-15 na 20-14.
Robo ya tatu Noela Renatus na Boke Juma wanaoichezea Vijana walibadilisha mchezo huku wakitumia mtindo wa kuingia ndani na mpira katika eneo la goli la DB Troncatti na kufunga, jambo lililofanya ipate pointi 18-9, 15-10.
Noela Renatus wa Vijana aliongoza kwa kufunga pointi 15 akifuatiwa na Boke Juma aliyefunga 14. Kwa upande wa DB Troncatti alikuwa ni Tumwagile Joshua aliyefunga pointi 15 akifuatiwa na Jesca aliyefunga pointi 13.
Wakati huo huo tIMU ya Wavuja Jasho imeifunga Lake Side kwa pointi 100-46 katika mchezo wa robo fainali wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Kigoma uliofanyika katika Uwanja Lakeside mjini Kigoma.
Kwa matokeo hayo Wavuja Jasho imeingia moja kwa moja fainali baada ya Kibondo na Kasulu kujiondoa katika nusu fainali.
Akizungumza na Mwanasposti, katibu wa Chama cha Kikapu Mkoa wa Kigoma, Aq Qassim Anasi alisema baada ya timu ya Wavuja Jasho kushinda itacheza na TBT kwa mfumo wa mara tano maarufu kama ‘best of five play off’.
Akizungumzia timu zilizojiondoa alisema walipewa taarifa ya barua kujiondoa kwao iliyoeleza kuwa ni kutokana na majukumu aliyonayo ya ujenzi wa uwanja.
“Unajua timu hizo zinatoka mbali. Kutoka hapo walipo mpaka kwenye mashindano kila timu inatumia Sh300,000 kwa usafiri,” alisema Anasi.
Vijana Queens ilivyoifumua DB Troncatti bdl