WAZIRI JAFO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI TANZANIA


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe.Guiseppe Sean Coppola na ujumbe wake katika Ofisi ndogo ya Wizara Jijini Dar es Salaam, Septemba 30,2024.

Mazungumzo hayo yamelenga kuongeza ushirikiano wa kibiashara hasa katika biashara ya mazao ya kilimo ikiwemo kahawa , pamoja na kubadilishana elimu na teknolojia na ushiriki katika Kongamano la biashara baina ya Italia na Tanzania pamoja na kuendeleza ushiriki katika Maonesho ya Biashara ya Sabasaba.

Related Posts