Baada ya kulisimamisha gari, tuliingia ndani. Nilimuona mama yake. Alikuwa amekaa sebuleni. Alikuwa mwanamke mnene na mfupi. Nilimkadiria umri wake kuwa ulishafikia miaka themanini.
Alikuwa amevaa dera na alikuwa amevaa hijab.
Baada ya kumuamkia. Mustafa alimwambia hapo hapo.