Mkaguzi kata ya Kisangura azidi kupeleka furaha kwa wananchi

Mkaguzi kata ya Kisangura Wilayani Serengeti Mkoa wa Mara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/Insp Genuine Kimario amezidi kupeleka furaha kwa wananchi anaowahudumia katani hapo kwa kutoa viti mwendo kwa wananchi wahitaji.

Mkaguzi huyo amebainisha kuwa ameendelea kutoa viti mwendo hivyo kutokana na changamoto aliyoikuta kwa wananchi anao wahudumia ambapo aliwaomba wananchi watakao guswa kuwasaidia kundi hilo lenye changamoto za miguu huku akiendelea kuwashukuru wananchi waliojitokeza tangu alipotoa viti mwendo kwa wananchi wa kata yake na wananchi kuona kupitia mitandao ya kijamii na kumuunga mkono kwa kutoa viti vingine kwa wananchi anaowahudumia.

Aidha Mkaguzi Kimario amebainisha kuwa nifuraha yake kuona wananchi wanaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kitendo kilichopelekea kuendelea kudhibiti uhalifu katani hapo huku akizidi kuwaomba ushirikiano zaidi wananchi hao ili amani na utulivu vitawale katika kata hiyo.

Sambamba na hilo amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu huku akihaidi kujitoa kwake kama dhamana yake kwa wananchi juu ya ulinzi wao na mali zao.

Related Posts