WADAU WA JOTOARDHI KUKUTANA TANZANIA

Meneja Makuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC),Mathew Mwangomba, akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 2,2024 jijini Dodoma kuelekea kwenye Kongamano la 10 la Jotoardhi Afrika litakalofanyika kuanzia Oktoba 21 hadi 27,mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WIZARA ya Nishati kwa kushirikiana na Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maziringira (UNEP), imeandaa kongamano la 10 la Jotoardhi Afrika (ARGeo-C10) litakalofanyika nchini kuanzia Oktoba 21 hadi 27 mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 2,2024 jijini Dodoma na Meneja Makuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC),Bw. Mathew Mwangomba,amesema kuwa  kongamano hilo linatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Bw.Mwangomba amesema kuwa kongamno hilo litashirikisha washiriki kati ya 700 hadi 1,000 kutoka nchi 13 zikiwemo za Afrika na mataifa mengine ya ulaya na uarabuni.

“Kongamano hilo litafunguliwa rasmi Oktoba 23 mwaka huu na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, likiwa na kaulimbiu inayosema, Kuharakisha Maendeleo ya Rasilimali za Joto ardhi katika Afrika, Masoko ya Gesi ya Ukaa na Upiunguzaji wa Gesi ya Ukaa.

“Kaulimbiu hii inasadifu kwa kiasi kikubwa adhma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia, kama ilivyoanishwa katika mkakati aliouzindua Aprili mwaka huu,” amesema Bw.Mwangomba

Aidha ameeleza  kuwa mkakati huo una lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo amesema kuwa  kongamano hilo litafungwa Oktoba 25 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Bw.Mwangomba amesema  kongamano hilo litaangazia mada mbalimbali ambazo ni uzalishaji umeme kwa kutumia joto ardhi, matumizi ya moja kwa moja ya joto ardhi katika sekta ya kilimo na ufugaji hasa wa samaki.

Pia, amesema  mada zingine ni uhandisi wa visima vya jotoa rdhi na teknolojia mpya, njia za kupata ufadhili wa miradi ya nishati mbadala ikiwemo nishati ya jotoardhi, uchambuzi wa faida za kimazingira na kijamii katika maendeleo ya miradi ya joto ardhi.

Mada zingine ni utafiti na uendelezaji wa rasilimali za joto ardhi, sera na udhibiti katika sekta ya rasilimali ya joto ardhi, faida ya kimazingira na kijamii katika maendeleo ya miradi ya joto ardhi.

Aidha ameeleza kuwa katika kongamano hilo washiriki watapata fursa za kimafunzo kwa kutembelea na kujifunza kwa vitendo katika maeneo ya miradi ya jotoardhi ya Ngozi mkoani Mbeya na Songwe mkoani Songwe.

“Washiriki pia watapata maarifa ya kimataifa kwa kufahamu maendeleo ya miradi ya jotoardhi duniani na kupata ujuzi kutoka kwa watoa suluhisho kubwa wa kimataifa.”amesema 

Meneja Makuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC),Mathew Mwangomba, akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 2,2024 jijini Dodoma kuelekea kwenye Kongamano la 10 la Jotoardhi Afrika litakalofanyika kuanzia Oktoba 21 hadi 27,mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Meneja Makuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC),Mathew Mwangomba, akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 2,2024 jijini Dodoma kuelekea kwenye Kongamano la 10 la Jotoardhi Afrika litakalofanyika kuanzia Oktoba 21 hadi 27,mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Makuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC),Mathew Mwangomba (hayupo pichani) wakati atoa taarifa kuhusu  Kongamano la 10 la Jotoardhi Afrika litakalofanyika kuanzia Oktoba 21 hadi 27,mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Related Posts