DC Mvomero awataka polisi kuwasaka wafugaji waliomjeruhi mkulima.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Judith Nguli amewataka jeshi la Polisi Wilaya humo kuwasaka kikundi Cha wafugaji ambacho wanatuhumiwa kumvamia mkulima Juma Bakari 61) mkazi wa kata ya Mtibwa na kumjeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake

DC Nguli ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara Kijiji Cha Kunke Kata ya Mtibwa kilicholenga Kujadili changamoto migogoro ya ardhi inayohusisha wakulima na wafugaji.

Kikundi hicho kinadaiwa kuvamia usiku wa maneno kwenye shamva alilokuwa akilinda mkulima huyo Kisha kumjeruhi na kuingiza Mifugo shambani kinguvuna kulisha.

DC Nguli amesema Kila mfugaji na mkulima kuhakikisha kusajili mashamba yao ili kupata hati na kuingia kwenye kampeni ya TUTUNZANE yenye lengo kupunguza changamoto ya migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.

 

Related Posts