WAZIRI MKUU RASMI MKUTANO WA KUMI WA WADAU WA LISHE.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 03, 2024 anafunga mkutano wa Kumi wa Wadau wa Lishe unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Malaika Beach Resort, Jijini Mwanza.

lengo la Mkutano huo ni kudumisha dhamira ya pamoja ya Serikali na wadau katika kuongeza msukumo na uwekezaji katika kutekeleza Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe ili kukabiliana na changamoto za utapiamlo katika jamii, na kupokea tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe nchini kwa mwaka uliopita.

Pia, Mkutano huo umelenga kutoa fursa kwa wadau wa lishe kukutana, kujadiliana na kupata maelezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Kitaifa wa Lishe (2021/22 – 2025/26) uliouzinduliwa mwaka 2021.

Kaulimbiu ya mkutano huo ni ”Kuchagiza Mchango Zaidi Wa Wadau Wa Kisekta Ili Kudumisha Matokeo Bora Ya Hali Ya Lishe Nchini Tanzania”.



Related Posts