Mwakilishi kampuni ya tuzo za chapa bora Afrika.(Best Brand Awards Africa’) nchini, Zakayo Shushu akimkabidhi tuzo mwanamitindo Hamisa Mobeto wakati wa tuzo zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI na taasisi 100 zapata tuzo ya kutambuliwa kama chapa bora iliyojulikana kama best Brands Awads katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mlimani City Oktoba 6,2024.
Mwakilishi kampuni ya tuzo za chapa bora Afrika.(Best Brand Awards Africa’) nchini, Zakayo Shushu akizungumza katika uzinduzi wa tuzo hizo amesema kuwa wametambua Chapa 100 ambazo zinawakilisha chapa nyingine nyingi.
Amesema kuwa chapa hizo zinawakilisha sekta mbalimbali ambazo kwa leo hazijaguswa kwa leo wamezipongeza hizo kwasababu kuwakumbusha watanzania kwamba kuna jambo linakuja wakae tayari na macho kwaajili yao.
Amesema wamezitambua chapa hizo kwasababu zimefanya vizuri kwa 2023/ 2024 kutokana na jopo la wataalam na watafiti na wabobezi kuungana kwaajili ya kuzipima zile chapa ambazo zinatoa huduma ya kuzalisha bidhaa.
“Wataalamu hao wao wakapendekeza na kutoa maoni juu ya Chapa hizo kwasababu ni miongoni mwa Chapa ambazo zimepata nafasi leo ya kupongezwa, kuthaminiwa na kuonekana mchango wao wa kile wanachokifanya kwa watanzania.” Amesema Shushu
Amesema lengo ya kutoa tuzo kwa chapa hizo kutoa hamasha kwa jamii ya watanzania, wazalishaji, wafanyabiashara, wajasiliamali kujikita na kuongeza ubunifu, ubobezi na ufanisi katika utendaji wao kazi na uzalishaji wao.
Akizungumzia kasumba ambayo tunayo watanzania Shushu amesema kuwa kumekuwa na matumizi ya bidhaa, mifumo ya huduma kutoka nje ya nchi, lakini tunashindwa kutumia kutokana na kukosa ufanisi na ubora, lakini wapo watu ambao wanafanya vizuri sana katika huduma hizo hizo wanatakiwa kupongezwa.
“Ili kutoa hamasa kwa wengine lazima tuwapongeze kwa ufanyaji kazi wao kwa ufanisi na ubora hapa nchini.” Ameeleza
Akizungumzia suala la uchaguzi wa chapa bora zilizofanya vizuri, kwa wale ambao wanaangalia mtu kapataje tuzo. Shushu amesema kuwa kama mtu amefanya kazi vizuri katika sekta yake lazima tumpongeze na kujifunza kutoka kwake.
“Sisi Best Brand Awards tumelijua hilo ndio maana Chapa za ufunguzi hazikuwa naupigaji kura, ingawa mchakato ulipitiwa na wabobezi, watafiti na watu wenye uwezo mkubwa wa kuchambua masuala yanayohusiana na chapa za biashara katika sekta husika kwa kuchukua wataalamu wanaohusika.” Amesisitiza
Akitolea mfano wa sekta Shusu amesema kama ni sekta ya benki basi wataalamu na watafiti wa sekta za benki ndio wanafanya tafiti ya chapa bora inayostahili katika utoaji huduma kwa jamii.
Kwa upande wa Meneja wa Kanda wa Benki ya CRDB, Badri Iddy ambaye ameiwakilisha benki ya CRDB kuchukua tuzo katika sekta ya kibenki amesema kuwa kupata tuzo hiyo ni jitihada za benki hiyo bunifu Afrika kwa kuangalia jinsi wanavyofanya kazi kwa kuwa wapo tofauti na beki nyingine zinavyofanya kazi.
“Tumekuwa ni benki ya kwanza kufungua milango Afrika, teyari tumefungua tawi Burundi mpaka sasa ni miaka 10, pia tumefungua DRC Congo na bado tunaendelea kuona tunafanyaje kazi ili kwenda kufungua matawi katika nchi nyingine Afrika na Duniani, lakini kwa Tanzania tupo kila kona kidijitali zaidi.” Ameeleza Iddy
Pia amewakaribisha wateja wao kuendelea kutumia huduma zao kwa kutumia simu za mkononi kwani sio lazima kufika katika matawi yao.
Licha ya hayo amesema kuwa wanaungana na serikali katika kufanyaji nao kazi kwa karibu ili kutimiza ndoto ya serikali ili kumwona mtanzania mwenye kipato cha chini anakua na kipato cha kati na cha juu.
Akizungumzia sekta ya Bima, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Assemble Insuarance Tanzania, Tabia Masoud amewashukuru watoa tuzo kwa kuwatambua kuwa ni Bima inayotoa mchango wa bima katika nchi za Afrika mashariki.
“Tuzo hii inamaana kubwa sana kwa Wateja, wadau, washirika na watu wote tunashirikiana nao, tumetoa tuzo hii kwa wote kama zawadi kwani haikuwa rahisi kwanii Assemble kama brand ni mpya kwenye soko kwani imeanzishwa 2021 lakini kampuni ni ya muda mrefu katika soko la Afrika Mashariki.” Amesema Tabia