PANDENI MITI KWA MAZINGIRA BORA YA KUJISOMEA- WAZIRI MHAGAMA

Na Linda Akyoo -Moshi

WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama ameuagiza uongozi wa Shule ya Sekondari Dkt Asha Rose Migiro iliyopo Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kuotesha miti katika shule hiyo ili wanafunzi wa shule hiyo wapate mazingira mazuri,Safi na bora ya kujisomea.

Ameyasema hayo leo tarehe 07 Oktoba,2024 kwenye ziara ya kutembelea Shule hiyo ambapo ameweza kukaguwa majengo mapya ya madarasa na mabweni ya kidato cha tano na chasita.

Aidha amsifu mradi huo wa madarasa pamoja na mabweni na kusema kuwa umekuwa mradi namba moja kati ya miradi yote niliyo itembelea”.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Nurdin Babu, amesema l pamoja na Waziri Mhagama anashughulikia Afya lakini ametembelea miradi mingine kama vile Shule ambayo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi za maendeleo na kufafanua Sh.bilioni 915 zimepelekwa katika mkoa huo.

Awali Mkuu wa shule ya Dkt.Asha Rose Migiro ,Flaviana Sumawe ameishukuru serikali kwa kuongeza shule hiyo kwa kidato cha tano na chasita na kusema ukimwelimisha mwanamke umeelimisha Taifa zima.

Shule ya Sekondari ya Dkt Asha Rose Migiro ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na wanafunzi 361,shule ilipokea shilingi Milioni 429 kwaajili ya upanuzi wa kidato cha tano na chasita,huku lengo likiwa ni kutoa elimu kwa mtoto wa kike wa Kitanzania.




Related Posts