Hayo yamebainishwa leo tarehe 6 Oktoba, 2024 na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe Jabir Makame wakati akizungumza na wananchi alipotembelea banda la REA yanapofanyika maonesho hayo kwa msimu wa tatu mwaka huu kijiji cha Leshata wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Mhe. Makame ameeleza kuwa, majiko banifu ni rafiki na salama kwa afya ya watumiaji nchini na kuwasisitiza wananchi wake wayatumie kwa kuwa yanauzwa na kupatikana kwa bei rafiki.
Amesema Gairo inatekeleza kampeni ya URITHI WA KIJANI yenye lengo la kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ambayo yana athari katika Sekta ya Kilimo na Mifugo.
Ametaja wadau wanaoshiriki kuwa ni pamoja na Mashirika ya Mazingira, Kampuni za Gesi, Kampuni zinazotengeneza mkaa mbadala ikiwemo STAMICO, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira pamoja na Wizara ya Nishati.
Naye, Mhandisi wa REA Deusdedith Malulu ameongeza kuwa, majiko hayo yanatunza mazingira kwa kutumia kiasi kidogo cha mkaa na ufanisi wake ni mkubwa.
“Majiko haya hayaruhusu hewa ya mkaa ambayo ni hatari kwa watumiaji kutoka nje kwa aina ya muundo wake na hivyo kuwa rafiki kwa mazingira” amesema Mha. Maluku
Mha. Malulu amesema kupitia maonesho hayo wananchi wa wilaya hiyo wameanza kupatiwa majiko banifu na REA imeaza kutoa majiko 790 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.