SMZ YAIPONGEZA AIRTEL FOUNDATION NA IIT MADRAS KWA USHIRIKIANO

Na Nihifadhi Issa.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imesaini makubaliano na Serikali ya India katika kuhakikisha chuo cha International Institute Technology (IIT madras) kinafundisha na kutoa wataalamu kutoka Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa ameyasema hayo wakati akizindua Programu maalumu ya mafunzo inayobeba jina la Airtel Africa Fellowship Program inayoendeshwa kwa mashirikiano baina ya IIT Kampasi ya Zanzibar na Taasisi ya Airtel Africa Foundation huko Bweleo MKoa wa Mjini Magharib
Aidha amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawapongeza Airtel Afrika kuamua kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa sayansi kila mwaka kwani kufanya hivyo kutazalisha wasomi waliobebea kwa manufaa yao na ya Taifa.
Nae meneja wa Airtel Tanzania bwana Dinesh Balsing amesema Airtel imeamua kusaidia vijana wa Afrika kujifunza sayansi na Teknologia kwa ajili ya kupata ujuzi wa kuijenga kesho yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi na mawasiliano wa Airtel Bitric Ngalo amesema ni fursa kubwa kwa wanafunzi ambao watakao Pata alama za juu kwa wanafunzi wa sayansi Kutoka nchi za Afrika.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliopata ufadhili huo kutoka Airtel Afrika Foundation Mwema Mumbwa amesema fursa hiyo sio tu itawanufaisha wao bali hata familia zao, Nchi za Afrika pamoja na kutanuka kwa Tasnia nzima ya Sayansi na Teknolojia
Airtel Africa Foundation itaendesha program hiyo ya kuwapata wanafunzi ufadhili ya kusoma katika chuo cha IIT Madras kapasi ya Zanzibar kwa kila mwaka na itajumuisha nchi 14 za Africa ikiwemo Tanzania
Kwa mwaka wa masomo 2024/2025 jumla ya wanafunzi kumi kutoka nchi za Tanzania, Kenya na Zambia walioanza masomo yao ya Shahada ya Kwanza katika fani za Sayansi ya Data na Akili Bandia watafaidika na program hiyo.

Related Posts