Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdul Mhinte katikati akiwa katika picha ya pamoja katika Maadhimisho ya Kichaa cha Mbwa Duniani Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza Septemba 28, 2024.(Picha na Faustine Gimu)
Jina na njia za kuambukizwa
Dkt. Stanford Ndibalema Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Jamii ya Veterinari kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi akiwa katika picha ya pamoja baada ya kushiriki zoezi la kutoa elimu kuhusu Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa pamoja na kuchanja Mbwa katika Kijiji cha Mwalobagole Wilaya Misungwi Mkoani Mwanza Septemba 27, 2024 .
Dalili za ugonjwa
Tiba na kinga
Kila ifikapo tarehe 28, Septemba kwa kila Mwaka Tanzania huungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha Siku ya Kichaa cha Mbwa.
Kwa hapa Tanzania Maadhimisho haya mwaka huu yalifanyika Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdul Mhinte alisema zaidi ya watu elfu sitini duniani kote hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Kichaa cha mbwa kila mwaka.
“Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya watu elfu sitini hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa”amesema .
Aidha, amesema kwa mujibu wa Wizara ya Afya, watu elfu moja na mia tano Tanzania hufariki dunia kutokana na ugonjwa huo na asilimia hamsini ni watoto wanaoathirika na ugonjwa huo kila mwaka .
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdul Mhinte akizungumza katika Maadhimisho ya Kichaa cha Mbwa Duniani katika Uwanja wa Amani Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza Septemba 28, 2024(Picha na Faustine Gimu)
Halikadhalika Bw. Mhinte alitoa wito kwa jamii kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.
“ Tuendelee kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwapatia chanjo wanyama kwani Wanyama wafugwao kama vile mbwa,paka, ng’ombe,kondoo mbuzi na wanyamapori kama vile fisi, nguchiro, mbwamwitu na mbweha wanaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa”alisema.
Je, ni maeneo yapi ya mwili uking’atwa na mbwa mwenye kichaa cha mbwa mbwa Maambukizi yanaenda kwa kasi zaidi?
Dkt. Stanford Ndibalema Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Jamii ya Veterinari kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi alisema kuwa Mtu aking’atwa na mbwa mwenye kichaa cha mbwa sehemu za karibu na kichwa mfano kwenye mikono, mabegani au kichwani ni rahisi kupata ugonjwa wa kichaa cha mbwa kuliko aliyeng’atwa mguuni.
Afisa Mifugo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Philemon Katabazi akitoa Elimu kuhusu Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa katika Shule ya Sekondari Jitihada Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza tarehe 27, Septemba, 2024.
Aidha, Dkt. Ndibalema alisema pindi mtu anapong’atwa na mbwa mwenye ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa ni muhimu kuchukua maji mengi na kukisafisha kidonda na sabuni huku akizungumzia ushirikiano wa kisekta katika kupambana na magonjwa yaenezwayo kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.
“Magonjwa yaenezwayo kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu tunayadhibiti kwa dhana ya afya moja, ushirikiano baina ya Sekta ya Afya , Sekta ya Mifugo,na tunawatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika utoaji wa Elimu kuhusu ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa na namna ya kujikinga”alisema.
Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Jamii ya Veterinari kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Stanford Ndibalema akikabidhi Kipeperushi(Kibango) kwa Kaimu Mkuu Shule ya Sekondari Misungwi Wilayani Mishungwi Mkoani Mwanza Bw. Ramadhan Nassoro chenye ujumbe Mahsusi kuhusu Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa tarehe 27,Septemba, 2024.
Kuhusu suala la matunzo kwa wanyama Dkt. Ndibalema alisema wanyama kama vile mbwa wanahitaji maji, chakula, nyumba ya kupumzikia ili wasizagae ovyo na kuleta madhara kwa binadamu.
Pia, Dkt. Ndibalema aliikumbusha jamii umuhimu wa kupiga namba 199 bure kwa elimu zaidi kuhusu ugonjwa wa kichaa cha mbwa ambayo ni namba kutoka Kituo cha huduma kwa wateja cha Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma.
Katika suala la imani potofu Dkt Ndibalema ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kukimbilia kwa waganga wa Tiba Asili pindi inapokubwa na changamoto ya kung’atwa na mbwa mwenye kichaa cha mbwa na badala yake kwenda hospitalini kwa matibabu zaidi.
Mratibu wa Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Baltazar Gasper alisema kuna umuhimu mkubwa kwa sekta zote kushirikiana kupambana na ugonjwa wa kichaa cha Mbwa.
“Udhibiti wa ugonjwa wa Kichaa cha mbwa ni suala la mtambuka linalohitaji ushiriki wa pamoja wa sekta zote na wadau kuanzia ngazi ya jamii hadi kitaifa na kaulimbiu ya mwaka huu inalenga dhana ya afya moja katika kuondoa vikwazo na kuongeza ufanisi katika udhibiti wa magonjwa yaenezwayo kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu”alisema.
Mratibu wa Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Baltazar Gasper akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani tarehe 28, Septemba, 2024 katika Uwanja wa Amani Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Mhe.Johari Samizi alitoa wito kwa wananchi kuwa na desturi ya kuchanja mifugo yao .
“Wale ambao hawajachanja mbwa wao wajitokeze kwa wingi kuchanja ili kujikinga na kulinda afya ya binadamu asipate ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa na kulinda afya ya wanyama hao pia”alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Mhe.Johari Samizi akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani tarehe 28, Septemba, 2024 katika Uwanja wa Amani Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.(Picha na Faustine Gimu,Elimu ya Afya kwa Umma)
Elimu kuhusu Kichaa cha Mbwa ikitolewa katika Shule ya Sekondari Jitihada Septemba 27, 2024.
Nini Mtazamo wa wananchi kuhusu Elimu ya Afya Juu ya Kichaa cha Mbwa?
Wananchi kutoka Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza walitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa kuwekajitihada kubwa katika kuelimisha jamii.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao akiwemo Gervans Kanuti, Stela Maganiko pamoja na Ntole Mungala walisema wamepata mafunzo muhimu kuhusu ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa na kusema hapo awali walikuwa wanafika mbwa na kuondoa dhana potofu kuwa mbwa hulogwa.
“Kipindi cha nyuma nilikuwa naficha mbwa wasichanjwe naleta mmoja tu wengine wanabaki nyumbani pia nilikuwa nina imani potofu kuwa mbwa aking’ata mtu atakuwa amelogwa hivyo tumebadilika na mtu akiumwa na mbwa ni muhimu kwenda hospitalini”alisema Kanuti .
Ikumbukwe kuwa Maadhimisho ya Kichaa cha Mbwa Duniani Elimu ilitolewa kwa Jamii na Shule ikiwemo Shule ya Sekondari Misungwi na Shule ya Sekondari ya Sekondari Jitihada,vyombo mbalimbali vya habari na huduma za kuchanja mbwa ilitolewa ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wadau ikiwemo Shirika la Chakula Duniani (FAO) na Shirika la Msaada la Watu wa Marekani (USAID) na yalikwenda sambamba na kaulimbiu isemayo”Ondoa Vizingiti vinavyokwamisha Mapambano dhidi ya Kichaa cha Mbwa”
Kido wa “Holelaholela itakukosti (aliyevaa katuni ya rangi nyekundu)akitumbuiza katika Maadhimisho ya Kichaa cha Mbwa Duniani.
Msanii akichezea nyoka katika Maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani Septemba 28, 2024 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.