WADAU WAJENGEWA UWEZO NAMNA YA KUSIMAMIA SHERIA NA MIONGOZO YA MAAFA

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amesema Sheria na Miongozo ya Maafa ni lazima isimamiwe na kutekelezwa kikamilifu kwani ndiyo njia pekee ya kupunguza madhara ya maafa

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 07 Ocktoba, 2024 Jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga, wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa maafa kwa Waratibu wa maafa wa Wizara na Taasisi, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Kimataifa na Asasi za Kiraia.

Ameeleza kwamba Juhudi za kijamii na ushiriki wa wadau ni nguzo muhimu katika usimamizi wa maafa yanayotokea yanayotokea na yanayoweza kutokea ikiwemo tetemeko la ardhi, mafuriko, mkame, maporomoko ya ardhi, ajali za majini na nchi kavu.

Naibu Waziri huyo amesema, “ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatakuwa na mafanikio zaidi endapo suala la usimamizi wa maafa litapewa kipaumbele kwa kuingizwa katika mipango na programu za maendeleo katika maeneo yetu na pia kwa kutumia vyema maarifa na ujuzi mtakaopata hapa ili kuimarisha hatua za tuzuia na kupunguza madhara ya majanga.

Aidha mafunzo hayo ni hatua ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama tawala ya Mwaka 2020 – 2025 ambayo katika Ibara ya 107 inaelekezwa Serikali kuchukua hatua za kuimarisha mifumo ya utendaji ya wizara, taasisi na mamlaka za serikali za mitaa ikiwemo kutoa elimu ya usimamizi wa maafa.

“hatua ya kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa ya aina mbalimbali kwa kushirikiana na wadau imelenga kuokoa maisha ya watu, kupunguza upotevu wa mali na uharibifu wa miundombinu alisema,”

Nae, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Eleuter Kihwele, amesema kuwa, mafunzo hayo yanayotolewa kwa siku mbili yataleta mchango katika kukabiliana na masuala ya majanga nchini.

Related Posts