Mwenyekiti wa Taasisi ya Utu Kwanza Shehzada Walli akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichana Oktoba 6,2024 katika Utu Run iliyoanzia na kumalizika Viwanja vya Farasi Oysterbay Jijini Dare es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Utu Kwanza Shehzada Walli akiwa amesimama meza kuu mbele ya mgeni rasmi ambaye amemwakilisha Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani Hamad Masauni ambaaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Huduma za Uangalizi wa Wafungwa wa Kifungo Cha Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Francis Nsanze kabla ya kumkabidhi zawadi maalumu kutoka Utu Kwanza kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam 06,Oktoba, 2024.
Wakimbiaji wa Km60 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Wa Idara ya Huduma za Uangalizi wa Wafungwa wa Kifungo Cha Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Francis Nsanze.
Mtangazaji wa Habari za Michezo Kituo Cha ITV na Radio One ambaye pia alikua mkimbiaji wa mbio za baiskeli Km120 Amri Massare akiteta jambo na Mwenyekiti wa Utu kwanza Shehzada Walli mara baada ya kuasili katika Viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi wameichangia Taasisi ya Utu Kwanza Mil.2 ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada za Taasisi hiyo katika kutoa msaada wa Kisheria kwa wananchi walioko Mahabusu na Magerezani nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka miwili ya Taasisi ya Utu kwanza aliyekuwa mgeni rasmi
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uangalizi wa Wafungwa wa Kifungo Cha Nje kutoka Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Charles Francis Nsanze amemwakilisha Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni na amemkabidhi mchango wa Mil.2 kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Utu Kwanza Shehzada Walli.
Akizungumzia kuhusu fedha zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani amesema ni kwa ajili ya kuchangia dawati la utoaji wa huduma za kisheria kwa wafungwa na mahabusu nchini ambao hawana uwezo.
Nsanze amesema kuwa jamii wanapaswa kuwa na ufahamu mkubwa kuwa ndugu zao walioko Magereza ipo siku watarudi uraiani baada ya kumaliza vifungo vyao hivyo waache tabia ya kuwatenga kwani wengi ambao wamemaliza vifungo vyao pindi wanaporudi uraiani ndugu na jamaa zao huwatenga na kuwanyima haki ya kuishi kwa amani huku wakichangia kuwasababishia msongo wa mawazo.
“Wafungwa wengi wanaporudiuraiani baada ya kumaliza vifungo vyao wengi hukumbana nai yanyapaa,kukosa ajira jambo ambalo wengine hulazimika kufanya matuko ya uhalifu na kurudi tena Gerezani wanakoona ndiyo sehemu sahihi kwao kuishi jamii wanapaswa kupewa elimu ya kuishi kwa upendo bila kuwatenga ndugu zao walio fungwa na kumaliza vifungo”amesema Nsanze.
“Jamii ,Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu na Viongozi wa dini wa made hebu yote wanao wajibu wa kutoa elimu ya kuacha unyanyapaa kwa ndugu zao ambao walikua wafungwa na kuishi vizuri pindi wanaporudi uraiani” amesema Nsanze.
Mbio hizo za ‘Utu kwanza Run’ zimefanyika kwa mara ya pili ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kuchangia fedha za kusaidia msaada wa dawati la kisheria kwa watu wasiokuwa na uwezo waliopo Magereza na Mahabusu.
Hafla hiyo imepambwa na mbio za baiskeli za 120Km huku 60Km. zilizoanzia Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani hadi Viwanja vya Farasi vilivyopo Ostarbay Jijini Dar es salaam ambapo washiriki wengine wamekimbia 21Km. mbio za 10Km na 5 Km
Wakati huohuo Walli amesema kuwa wanahitaji kiasi cha
Mwenyekiti wa Taasisi ya Utu Kwanza ambaye pia ni Mratibu wa ‘Utu Kwanza Run’ ShahzadaWalli amesema kuwa ndani ya mwaka mmoja tangu walipoanza kutoa huduma hiyo kwa watu ambao hawana uwezo wa kujitetea walioko Mahabusu na magerezani wamefanikiwa kusaidia Watanzania 300 kwa kutoa huduma hiyo.
Aidha Wali amesema kuwa katika mafanikio hayo ndani yake kuna changamoto zimejitokeza kwa sababu Mahakama imesitisha wao kwenda Magerezani na Mahabusu kuzingumza na wahitaji ili waweze kuwapa msaada wa Kisheria.
Mwisho amewashukuru wadhamini ambao ni Meru,ASAS