Bashungwa apiga marufuku kuzidishwa kwa abiria na uzito kwenye vivuko

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa ameutaka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) pamoja na vyombo vingine vya usafiri ndani ya maji kuzingatia sheria na miongozo mbalimbali ya usalama kwenye vivuko kwa kuhakikisha hawazidishi abiria wala mizigo ili kulinda usalama wa abiria pamoja na mali zao.

Bashungwa ametoa maelekezo hayo Mkoani Lindi wakati akizungumza na Wananchi na kutolea mfano ajali iliyotokea Oktoba03, 2024 nchini Congo ambapo Meli MV Merdi ilizama katika Ziwa Kivu na kusababisha vifo na upotevu wa mali.

“Ni marufuku kwa TEMESA kujaza abiria na mizigo kupita viwango, abiria msikubali kupanda chombo ambacho umeambiwa ujazo umepita ukomo na msiwe wabishi kwani tunafanya hiyo kwasababu tunataka kulinda nguvu kazi ya Taifa letu”, amesisitiza Bashungwa.

Bashungwa ametoa rai kwa wananchi kuwa na subra ya kusubiri kivuko kingine pindi wanapoona Kivuko kimejaa ili kuepusha ajali na matukio kama hayo na kuhakikisha tunalinda na kutunza nguvu kazi ya Taifa.

 

Related Posts