Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati) na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadiliana masuala mtambuka yanayohusu ushirikiano kati ya Tanzania na Italia katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tatu kushoto), Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda Ezekiel (wa pili kulia), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine (kushoto), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise (kulia) na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Clementine Msafiri (wa pili kushoto).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kulia), akiongoza kikao alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola, kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali zikiwemo fursa za kiuchumi zilizopo katika ushirikiano wa Tanzania na Italia. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda Ezekiel, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
atibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola (hawapo pichani) walipokutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali zikiwemo fursa za kiuchumi na kijamii zilizopo ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa Tanzania na Italia. Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda Ezekiel, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa tatu kulia), akiongoza kikao alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola, kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali zikiwemo fursa za kiuchumi na kijamii zilizopo nchini ikiwa ni hatua ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa Tanzania na Italia. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili kulia), Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda Ezekiel (wa pili kushoto), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine (wa tatu kushoto), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise (wa kwanza kulia) na Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Jabir Selemani (wa kwanza kushoto)
Balozi wa Italia nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola, akizungumza wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali zikiwemo fursa za kiuchumi zilizopo nchini ikiwa ni kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Italia. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda Ezekiel, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Na. Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa wito kwa wawekezaji kutoka nchini Italia kutumia mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini kuwekeza mitaji yao katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ili kukuza uchumi wa pande hizo mbili.
Dkt. Nchemba ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Giussepe Sean Coppola, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeweka vivutio mbalimbali vya uwekezaji na kuialika sekta binafsi ya Italia, kushirikiana na Serikali kwa kuwekeza katika ujenzi na uendeshaji wa miradi mbalimbali hapa nchini ukiwemo mradi wa Reli ya Kisasa wa SGR.
Kwa upande wake, Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Giussepe Sean Coppola, alimwagia sifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia vizuri uchumi na maendeleo ya nchi ikiwemo kuunda tume ya kushughulikia changamoto za kikodi nchini.
Alisema kuwa anaamini matokeo ya Tume hiyo yataongeza chachu ya kufanyabiashara na uwekezaji hapa nchini hatua itakayochochea ajira, ukuaji wa uchumi na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika kuchochea maendeleo ya nchi.
Aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa kuchangia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo kwa kuendeleza mnyororo wa thamani wa zao la kahawa chini.
Italia imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania kwa kufadhili miradi mbalimbali kupitia bajeti kuu ya Serikali, ikiwemo miradi ya maji, afya, mafunzo ya ufundi stadi na huduma katika sekta za utalii na hoteli, uchumi wa buluu na usawa wa kijinsia.