FEZA SCHOOLS YANOGESHA MAONESHO YA TEKNOJIA,YAPIGA HODI KANDA YA ZIWA

Na Mwandishi wetu Geita.

WAKATI Maonesho ya Saba ya teknolijia ya madini yakiendelea mkoani Geita kamapuni mbalimbali zinashiriki maonesho hayo zikiwemo zinazosambaza bidhaa za migodini hasa wauzaji wa magari pamoja na mitambo.

Kwa mwaka huu kitu cha kipekee ni ushiriki wa shule binafsi katika maonesho hayo.Miongoni kwa shule hizo ni za Waja na Savannah Plain ambazo zinatoka kanda ya ziwa pamoja na shule za FEZA

Katika Banda la Shule ya FEZA huduma wanazozitoa ni pamoja na usahili wa wanafunzi kwa kidato cha kwanza kwa muhula mpya wa masomo wa 2025

Akizungumza katika maonesho wakati wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari mkoani Geita walipotembelewa banda lao kwa lengo la kujifunza Ofisa Mratibu na Msaili wa wanafunzi wa FEZA ,Huzaifa Sizya amesema wao wamejikita katika kutoa elimu bora na zeye viwango vya kimataifa kwa shule zenye mtaala wa Kimataifa (Feza International).

Ameongeza kuwa pamoja na viwango vya kitaifa chini ya NECT na kusisitiza FEZA imekuwa ikiongoza katika matokeo ya Kidato cha Nne na Sita kwa miaka yoote ikijivunia rekodi ya kutoa daraja la kwanza kwa wanafuzi woote miaka zaidi ya 10 sasa

Pia ameema FEZA iko mbioni kufungua shule kanda ya ziwa ili kuwaletea wananchi na wazazi huduma jirani na kuunga mkono juhudi za serikikali kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora na si bora elimu.

“FEZA ina mpango wa kuwasomesha bure wanafunzi ambao wanauwezo wa kimasomo darasani lakini kutokana na changamoto za familia hawana uwezo wa kusomeshwa, hivyo wanafunzi wenye changamoto hizo hupata ufadhili hasa wale wenye uwezo mkubwa katika masomo ya Sayansi ili kutengeneza madaktari na Wahandisi wa kada mbalimbali.”.

Related Posts