SOUWASA YAJITOKEZA KUTATUA KERO YA MAJI RUHUWIKO NA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

 Wakazi wa Mtaa wa Ruhuwiko Kanisani Kata ya Ruhuwiko Manispaa ya Songea, wameipongeza mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) kufika eneo hilo kusikiliza kero mbalimbali zinazohusu maji pamoja nakutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya maji.

Wametoa pongezi hizo Mara baada ya kutembelewa na timu ya wataalamu kutoka SOUWASA waliokita kambi mtaani hapo hii leo, katika utekelezaji wa kampeni ya SOUWASA mtaa kwa mtaa iliyolenga kuwafikia wateja wao katika kipindi hiki ya wiki ya huduma kwa wateja, ili kukutana moja kwa moja na wateja kusikiliza kero zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi, pamoja nakuwarahisishia kupunguza gharama za usafiri kuwafata ofisini.

Akizungumza baada yakupata elimu na ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili, Gordian Haule ameeleza namna ambavyo alivyofurahishwa na SOUWASA ilivyoweza kutambua umuhimu wa wateja wao nakuamua kuwafata maeneo walipo, huku akitoa rai kwa Mamlaka kufanyia kazi maombi waliyoyaomba ili kudumisha ushirikianao baina yao na wateja wao.

Akieleza kuhusiana na changamoto kubwa iliyowasilishwa na wateja wengi kuhusiana na Ankara za maji kuwa juu ukilinganisha na matumizi, Juma Mwakaje mkuu wa Kanda kitengo cha Biashara kutoka SOUWASA, amesema sababu inayoweza kuchangia bili ya maji kuwa kubwa ni mivujo mbele ya mita, inayopelekea mita kusoma masaa 24 pasipo mteja kufahamu, hivyo kama mamlaka pindi wanapofahamu changamoto hiyo humshirikisha mteja moja kwa moja, nakuhakikisha wanafika haraka kulitatua tatizo hilo.

Aidha ameeleza kuwa  wameweza kubaini kwamba changamoto iliyopo kwa wateja wengi wameshindwa kudhibiti kiwango cha matumizi ya maji kwa kudhani ujazo wa ndoo moja ya maji ni Sawa na Lita 20 jambo ambalo nikinyume kwani inatakiwa kipimo cha ujazo wa maji kipimwe kama yalivyo mafuta yanavyouzwa kwenye ndoo ili kuleta uhalisia wa Lita hizo.

Mhandis uzalishaji na usambazaji kutoka SOUWASA Charles Mathias Kitavile, amesema ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Songea kukutana na wateja wao imelenga kufahamu changamoto zinazowakabilu wateja ili kuzitafutia ufumbuzi huku matarajio yao nikuhakikisha maeneo yote ambayo hayajaunganishwa na mtandao wa maji yanafikiwa na huduma hiyo.

Related Posts