TCB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, YAWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA

BENKI ya Biashara Tanzania(TCB) imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kuwakaribisha wafanyabiashara kutumia huduma zao ili kuweza kukua zaidi kwakuwa wapo mbioni kujiunga na  soko la hisa.

Akizungumza katika hafla hiyo leo Oktoba 8,2024 Mkurugenzi w Biashara kwa Wateja Wadogo na Wakati wa TCB Lilian Mtali amesema miongoni mwa mikakati yao ya hivi karibuni ni pamoja na kuipeleka benki hiyo kwenye soko la hisa hivyo ni muhimu kwa wateja kujitokeza na waliopo kujiandaa kuwa sehemu ya wanahisa.

“Tunategemea kuipelekea TCB kwenye soko la hisa hivyo hata mliopo humu naamini miongoni mwenu mnaweza kuwa wana hisa hivyo naomba tuwe karibu ili punde suala hili lutakapokuwa teyari mchangamkie fursa zakuwekeza na kuwa wanahisa,”amesema Mtali.

Amesema wiki ya huduma kwa wateja ni muhimu kwa benki hiyo kwakuwa pamoja na mambo mengine imejielekeza katika kutambua na kuthamini mchango wa wateja.

“Wateja ni muhimu katika ukuajo wa benki yetu  kwa sasa lengo leti ni kuhakikisha TCB inakuwa miongoni mwa benki tatu zinazoongoza nchini,”amesema.

Amesema wiki ya mteja itaonyesha dhamira yakutoa huduma bora kwa mteja pamoja na kujenga imani na mahusiano yakibiashara.

Naye mteja mkongwe wa benki hiyo  ambaye ni Mkurugenzi wa UBX Tanzania Limited Seronga Wanguf amesema  pamoja na huduma nzuri zinazotolewa bado wana changamoto  kutuma miamala kimataofa pamoja na kuhamisha pesa kwenda kwenye mabenki mengine.







Related Posts