Wakulima Nchini washauriwa kujiunga na Ushirika na kutumia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde amewataka wakulima nchini kujiunga Katika Vyama vya ushirika ili kunufaika kupitia sekta ya kilimo na kukabiliana na changamoto za masoko pindi wanapotaka kuuza mazao yao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Samia Kilimo Expo msimu wa tatu Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Mhe.Silinde amesema Serikali inadhamira njema na wakulima hivyo ni vyema wakajiunga Katika ushirika ili kuuza mazao Yao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umekuwa na mafanikio makubwa.

Silinde amesema tangu kuanza kwa ushirika nchini umeonekana kuwa na tija Kwa wakulima ambao waliokuwa wanauza Kwa bei ya chini nna vipimo visivyozingatia mizani

“nimeambiwa hapa Gairo Kwa mwaka mmoja jumla ya vyama vya ushirika 13 vimesajiliwa kupitia Vyama ushirika haya ni matokeo mazuri Sana ”

Kwa upande wake Naibu Mrajis (Uhamasishaji) Tume ya Maendeleo ya ushirika Tanzania (TCDC) Consolata Kiluma amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuona umuhimu wa kujiunga na Vyama vya ushirika .

Amesema, moja ya changamoto wanayokutana nayo ni matumuzi ya vipimo mizani ambapo Kwa Sasa wanahakikisha Kila Mkulima ananufaika kupitia sekta ya kilimo.

Anasema baadhi ya wafanyabiashara wanapita Kwa wakulima Moja Kwa Moja na kununua Mazao Kwa kutumia vipimo vusivyo rasmi

Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabiri Makame amesema hii ni mara ya tatu tangu kuanza kufanyika kwa maonesho hayo ya Kilimo Ngazi ya Wilaya.

Makame amesema lengo la maonesho hayo ni kuwafikia wakulima wa chini Ngazi ya kata na Kijiji ambao wengi wao hushindwa kusafiri kwenda Morogoro Mjini yanayofanyika maonesho ya Kilimo na mifugo Ngazi ya mkoa maarufu kama nanenane.

Amesema kutambua hilo walianza kufanya maonesho hayo ambayo yameonsha kuleta matokeo chanya wakulima kubadili kutoka mfumo mazoea kuanza kulima kilimo cha kisasa.

Amina Semwenda ni mmoja wa wakazi wa Gairo amesema mfumo wa stakabadhi ghalani ni mzuri lakini elimu zaidi inahitajika kutambua umuhimu wake kwa baadhi ya wakulima ambao Bado hajajiunga na vyama vya Ushirika.

 

 

 

Related Posts