BASHUNGWA AMUAGIZA DKT MSONDE NA TBA KUFANYA UCHAMBUZI WA MFUMO KUJENGA NYUMBA ZA WATUMISHI KWA GHARAMA NAFUU

 

Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze Septemba 9, 2024

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb), amemuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, pamoja na Wakala wa Majengo ya Watumishi wa Umma (TBA) kufanya uchambuzi wa mfumo katika kujenga nyumba za watumishi kwa gharama nafuu.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba nane za wakuu wa idara wa Halmashauri ya Chalinze, mkoani Pwani, zilizogharimu sh. milioni 960.5, Bashungwa ameielekeza TBA kuwa wabunifu katika kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za watumishi.

Amemtaka Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na TBA wafike Chalinze kujionea na kujifunza katika ujenzi wa nyumba zao za kisasa ili kupata mbinu bora za kuboresha na kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba hizo.

Aidha, Waziri Bashungwa amewataka watumishi kuwa wazalendo na kuacha urasimu wanapotoa huduma kwa wananchi .

Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa  amezindua soko jipya la Chalinze lililogharimu sh. bilioni 1.7 na kuwashauri wajasiriamali kuwa wabunifu katika kuanzisha biashara tofauti ili waweze kupata soko kirahisi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Miundombinu cha Halmashauri ya Chalinze, Injinia Olais Sikoi, ujenzi wa nyumba nane za wakuu wa idara ulianza mwaka 2022 na kufikia asilimia 98 kukamilika.

Related Posts