Raia hao wenye hasira baadhi ikiwa ni wale waliowapoteza wapendwa wao katika ajali ya boti Oktoba 3 mwaka huu , waliandamana leo asubuhi mbele ya chumba chakuhifadhia maiti mjini Goma.
Shughuli za usafiri wa umma zilikwama kwa masaa kadhaa kabla ya polisi kuutawanya umati huo uliotaka kupewa miili ya ndugu zao ambayo serikali ilikuwa imepanga kufanya hafla ya mazishi Jumatano lakini ikaziakhirisha kwa hadi siku ya Alhamisi wiki hii jambo ambalo limeongeza hasira kwa familia zilizo athirika.
“Hitaji letu nikupewa miili ya watu wetu lakini cha ajabu hatufahamu hata siku yamazishi kabisa. kwa hiyo tumekusudia kufanya maandamano ambayo ni njia tunayoitumia kuwashinikiza watukabizi miili ya watu wetu kama sio basi tutaandamano nakufunga barabara.”, alisema Olivier.
”Ninahitaji mwili wa ndugu yangu wiki moja hii sasa ,tumetaka kumuonesha gavana wetu kwamba tumeshikwa na hasira kwa hiyo anatakiwa kupata suluhisho kwa tatizo hili.”, alisikitishwa kwa upande wake Honorine.
Vyanzo vya ndani vimeeeleza kuwa marehemu hao 34 kama ilivyo hesabiwa na maafisa wa serikali walitakiwa kuzikwa, baadhi katika makaburi ya Makao wilayani Nyiragongo karibu na mji wa Goma na wengine katika mji wa Bweremana na Minova, mkoani Kivu Kusini.
“Roho yangu inauma sana”
Feza Ombeni ni mama mjane aliyewasili hapa kwenye chumba chakufadhi maiti lakini bado anahangaika kupewa miili ya wanawe wawili waliofariki katika ajali hiyo ya boti.
“Nilimpoteza mtoto na mjukuu wangu naomba mwili wa mtoto wangu nimfanyie mazishi mwenyewe ona sasa ni wiki moja roho yangu inauma saana”, alisema Ombeni.
Kwenye mazungumzo yake na vyombo vya habari , Prisca Luanda mshauri wa gavana wa kijeshi mkoani Kivu Kaskazini ahusikiaye na maswala yakijamii, amewapa ruhusa hata hivyo wale wanaotaka kuzibeba miili za wapendwa wao nakuahidi hafla ya mazishi kwa wote kama ilivyotakiwa na serikali
“Kwa wale wanaotaka kuzika watu wao tunawapa ruhusa na hivi miili hiyo inataka kutolewa kwa wenyeji. na kwetu kama serikali tutafanya mazishi ya watu alhamisi “, alisema Luanda.
Idadi kubwa ya waliofariki ?
Mapema mwanzoni mwa juma hili, ripoti iliyowasilishwa na maaafisa kutoka jiji kuu la Kinshasa na iliyoungwa mkono na majimbo mawili yalio athirika, inaonyesha takribani miili 34 iliyopatikana, manusura 80 na wengine makumi ya watu waliopotea.
Hadi kufikia sasa, juhudi zakujaribu kupata mabaki ya boti hiyo iliyoko umbali wa angalau mita 200 chini ya maji hazijafanikiwa .