TEA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA TABORA

Wanafunzi na wadau mbalimbali wakiendelea kujitokeza ili kuongeza uelewa juu ya utendaji wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yanayoendelea katika Viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora.

Hafla hii inatoa fursa nzuri kwa jamii kuelewa umuhimu wa elimu ya watu wazima na jinsi TEA inavyochangia katika maendeleo ya elimu nchini.

Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kujitokeza na kujifunza ili kuimarisha maarifa na ujuzi kwa maendeleo ya jamii zetu.




Related Posts