WATUMISHI MPAKA WA HOROHORO WAPONGEZWA KWA UKUSANYAJI MAPATO

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe.Mariam Ditopile ikitembelea Mpaka wa Tanzania na Kenya (Horohoro) wakiwa wameongozana na Mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Balozi Dkt. Batilda Burian na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) wakati wa Ziara ya Kamati hiyo Oktoba 9,2024.

……

Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, biashara, Kilimo na Mifugo imeridhishwa na utendaji kazi wa watumishi waliopo katika Mpaka wa Tanzania na Kenya (Horohoro) uliopo Mkoa wa Tanga kwa kukusanya mapato zaidi ya asilimia 100.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Mariam Ditopile kwaniaba ya Kamati hiyo walipotembelea Mpaka wa Tanzania na Kenya (Horohoro) katika Kituo cha kukusanya ushuru wa Forodha pamoja na kuona utendaji kazi wa Taasisi za Wizara ya Viwanda na Biashara hususani Tume ya Ushindani (FCC)  , Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  na Wakala wa Vipomo Tanzania (WMA) kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpaka huo.

Aidha Mhe.Ditopile ameagiza Wizara Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha kuhakikisha inaona namna ya kununua Scanner na Forklift ili kuimarisha utendaji kazi wa ukusanyaji ushuru kwenye mpaka huo ili kuongeza tija.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo ameahidi suala la upatikanaji wa nyenzo hizo kufanyiwa kazi huku akipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kufanya kwenye nyanja mbalimbali hapa nchini.

Akizungumzia Viwanda vilivyobinaglfsishwa ambavyo mpaka sasa vimeshindwa kufanya kazi, Mhe.Jafo amesema kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajiri wa Hazina, Serikali itaangalia namna ya kufanya kufufua Viwanda hivyo kutokana na ukweli kwamba Serikali ilikuwa na nia nzuri nyakati ilipoamua kuvibinafsisha.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe.Mariam Ditopile ikitembelea Mpaka wa Tanzania na Kenya (Horohoro) wakiwa wameongozana na Mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Balozi Dkt. Batilda Burian na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) wakati wa Ziara ya Kamati hiyo Oktoba 9,2024.

Ziara hiyo imelenga kutembelea na kuona utendaji kazi wa Taasisi za Wizara ya Viwanda na Biashara hususani Tume ya Ushindani (FCC) @fcc_tanzania , Shirika la Viwango Tanzania (TBS) @tbs_viwango na Wakala wa Vipomo Tanzania (WMA) @wakalawavipimotanzania kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpaka huo.

Related Posts