WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi,akizungumza leo Oktoba 9,2024 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).
WASHIRIKI wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, wakati akifungua kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi,amezitaka taasisi zote zilizopo katika masuala ya haki jinai nchini kuimarisha weledi katika shughuli zote za upelelezi.
Prof. Kabudi ameyasema hayo leo Oktoba 9,2024 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).
Prof.Kabudi amezipongeza taasisi hizo kwa kazi nzuri wanazozifanya kwa kutenda haki katika masuala ya haki hivyo niziombe taasisi zote zinazohusika na haki jinai kuongeza ufanisi pamoja na weledi katika kutenda haki.
“Nawapongeza kwa kuendelea kufanya kazi kwa weledi hivyo nawaomba mfanye kazi kwa kufuata taratibu na sheria na kanuni za nchi ili muendelee kumsaidia Mhe.Rais Samia Suluhu katika kutekeleza majukumu ya kila siku”amesema
Aidha, amesema kuwa taasisi hizo tatu zinapaswa kufanya mambo yao kwa mujibu wa sheria,taratibu na kanuni bila ya kuathiriwa na mihemuko ya kundi au mtu fulani.
“Fanyeni mambo yenu kwa weledi semeni mambo ambayo yapo tayari kusemwa kwa umma lakini kama jambo bado lipo kwenye uchunguzi endeleni kufanya uchunguzi bila kuathiriwa na kitu ama mtu yoyote yule”amesisitiza Prof.Kabudi
Vile vile, amewataka kuweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara ili kufahamia na kila mmoja kujua majukumu yake yanaishia wapi na ya mwenzake yanaanzia wapi ili kurahisisha uendeshaji wa mashauri na kutoa haki kwa wakati.
Hata hivyo Prof.Kabudi ametahadharisha kuwa 4R za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan zisitumike kama kivuli cha kuvunja sheria hivyo kuchochea uvunjifu wa amani nchini.
Amesema kuwa Rais Dk. Samia amepanua wigo wa utendaji haki nchini ikiwemo kuimarisha amani katika nchi yetu hivyo ni vyema 4R hizo zikatumika vizuri katika utekelezaji majukumu yao.
“Maana ya 4R ni kutekeleza yanayotakiwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za vyombo vinavyohusika na kusisitiza uzingatiaji utekelezwe kwenye hilo na kutahadharisha isiwe kichaka cha kuvunja sheria.”amesema
Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu mwakani Prof. Kabudi, ameziagiza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,TAKUKURU na Ofisi ya Upelelezi wa makosa ya Jinai kusimamia sheria ili uchaguzi huo uwe huru na wa haki.
“Navitaka vyombo vya upelelezi nchini kuhakikisha vinazingatia sheria na haki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwakani ili kudumisha umoja, amani na usalama wa nchi.”amesisitiza Prof.Kabudi
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Crispin Chalamila amesema kuwa kupitia utendaji wake ataendeleza ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa.
Amesema kuwa kwakuwa nchi inaenda kwenye uchaguzi Taasisi hiyo itahakikisha inasimamia sheria ili umoja na amani viendelee kudumu.
Naye Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Slyvester Mwakitalu, amesema kikao hicho ambacho kinakutanisha ofisi zinazounda utatu katika masuala ya haki jinai nchini lengo lake ni kujadili changamoto mbalimbali katika sekta hiyo pamoja na kuandaa mikakati ya kupata suluhu.
“Umoja wetu huu unajulikana kama Utatu lengo la kikao hichi ni hizi taasisi zetu tatu kukutana na kujadilina mambo mbalimbali ikiwemo changamoto zilizopo ambazo kwa namna moja au nyingine zinawanyika haki wananchi, kufanya tathimini ya mwaka mzima na kuweka mikakati ya mwaka ujao”amesema Mwakitalu
Awali Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai, amesema kuwa utendaji kazi kwa ushirikiano umekuwa na manufaa makubwa hivyo kutoa rai kwa taasisi hizo kuimarishwa kwakuwa kazi hiyo haiwezi kufanywa na moja.