ATE, CLOUDS NACOCACOLA WAUNGANA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

 Mkurugenzi mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni B, Nelson Saidi wakipanda mti mara baada ya kufanya usafi ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika wiki ya kwanza ya Oktoba kila mwaka.Wafanyakazi wa ATE na Cocacola wakifanya usafi katika barabara ya Cocacola Mikocheni B jijini Dar es Salaam leo Oktoba 11, 2024.

KATIKA kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na waajiri wa Clouds Group na Cocacola Kwanza, wamefanya usafi katika barabara ya kuanzia Mwenge hadi kona ya Cocacola na kupanda miti katika eneo lililopo mbele ya ofisi ya ATE.

Akizungumza leo Oktoba 11, 2024 jijini Dar Es Salaam mara baada ya kufanya usafi, Mkurugenzi mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran amesema kuwa wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka huu wameifanya kiutofauti.

“Hii imetokana na wiki ya huduma kwa wateja ikiwa na kauli mbiu ya Above and Beyond (⁶uduma zaidi)na katika kufanya hivyo ukiachilia ule wajibu wetu wa ATE ambao tumeendelea kuwafanya kuwa kwaajili ya waajili na wanachama wao kwa ujumla, lakini pia tumeona kwamba kutokana na kauli mbiu hiyo tutoke katika taratibu zetu za ndani tunazozifanya kila siku tuweze pia kujali mazingira ambayo tunafanyia biashara zetu. ” Amesema Suzanne

Akizungumzia kuhusiana na utunzaji wa mazingira, Suzanne amesema kuwa jambo hilo ni la msingi sana kwaajili ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho. ‘ Yatunze Mazingira na mazingira yakutuze.

“Sisi tumeona kwamba zoezi hili ni mhimu na tunataka kutengeneza utaratibu huu, ili tuendelee nao kwa miaka mingine.” Amesema

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni B, Nelson Saidi baada ya kupanda mti amesema kuwa kunatatizo la usafi wa mazingira kwenye jamii, kwa kufanya hivi itakuwa kama kengere kwa watu wengine, kampuni nyingine na wafanyabiashara ambao wanawafanya biashara katika mtaa wa mikocheni B kuiga mfano uliofanywa na ATE.

“Hatutaki tufanye kwa matukio, hatutaki mpaka kuwe na kitu ndio tufanye usafi.”

Amesema kuwa wanaratiba ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi mkoa wa Dar es Salaam kwa kila mkazi wa eneo lake anatakiwa afanye usafi kwenye eneo lake.

“Ufanyaji wa Usafi katika mazingira yetu itasaidia kupambana na changamoto za kimazingira… Kama mlivyoona mwaka huu tumepata mabadiliko ya tabia nchi, kumekuwa na mvua ambazo si za kawaida, kumekuwa na jua ambalo hatujazoea kuliona.

Amesema wakati wa eneo hilo wakiwa na taratibu za kufanya usafi, kupanda miti naamini kwa kiasi kikubwa tutaweza kukabiliana na changamoto za tabia nchini.

Licha ya hayo amewaomba wakazi wa Mikocheni B wawe na utamaduni wa kufanya usafi kwenye mazingira yao.

Akizungumzia masuala ya Afya, Afisa Afya Kata ya Mikocheni B, Adam Ndutu amesema kuwa ATE kwa kufanya usafi katika eneo la Mikocheni B wamefanya jambo kubwa kwa sababu usafi ni mhimu katika Maisha.

“Kukiwa na desturi ya kufanya usafi mara kwa mara tutaweza kuzuia magonjwa ya mlipuko lakini kampeni ya usafi ya ATE leo inaleta hamasa hata kwa jamii inayotuzunguka.” Amesema

Usafi huo umefanywa na ATE, Coca Cola Kwanza, Clouds Media Group, KFC (Dough Works Limited), DHL Tanzania na SGA Security.

Usafi ukiendelea.

Related Posts