AWESO AUSHUKURU UBALOZI WA TANZANIA BERLIN/UJERUMANI KUBEBA AJENDA YA MAJI


Berlin, Ujerumani

Waziri Aweso amehitimisha ziara yake nchini Ujerumani aipofika Berlin ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambapo ameushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kuratibu, kuwa kiuongo na kufanikisha ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutano wa Maendeleo Endelevu (Hamburg Sustainability Conference.

Aidha Waziri Aweso ametoa shukrani za dhati kwa Mhe Hassani Iddi Mwamweta Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na timu nzima ya Ubalozi kwa kumuwezesha pia kufanikisha kukutana na kufanya mazungumzo na vikao vya kimkakati na wadau wakubwa wa sekta ya Maji kwa nchi ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Facility – GCF), Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW), Shirika la Ujerumani la Ushirikiano wa Kimataifa (GIZ) na Kampuni ya Exponential Group.

Katika hatua nyingine. Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika wa kikao cha majumuisho, Waziri Aweso na Mhe. Hassani Iddi Mwameta, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani wamebainisha umuhimu wa sekta ya maji katika kuchochea maendeleo ikiwemo Diplomasia ya Uchumi.

Mwisho, Waziri Aweso amehimiza umuhimu wa Ubalozi kuwa daraja na kiungo imara katika kuhakikisha mipango yote na makubaliano yaliofikiwa na kujadiliwa na wadau hawa yanafuatiliwa, kuratibiwa na kuhakikisha yanaleta tija na kufanikisha ajenda ya Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Kumtua Mama ndoo Kichwani.


Related Posts