DC MPOGOLO AWATAKA TAHLISO KUKATAA KUTUMIKA

 Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo ameitaka Jumuia ya wanafunzi taasisi ya elimu ya juu Tanzania kutokubali kutumika.

Mpogolo ametoa wito uwo jijini dar es salaam katika ukumbi wa kareemjee wakati anafungua mkutano mkuu wa tahliso wenye lengo la kupitisha marekebisho ya katiba yao. 

Akizungumza na wajumbe wa mkutano uwo Mpogolo amewatahadharisha viongozi na wajumbe wa tahliso kutokubali kutumika kwa namna yoyote ili kutimiza malengo la mtu au kikundi.

Amesema uwepo wa jumuia hiyo ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kati ni daraja kati ya wanafunzi na viongozi wa serikali  kuu kufikisha changamoto zao kwa haraka na kutatuliwa. 

Ameongeza kuwa utulivu wa jumuia ya tahliso kwa sasa ni hatua kubwa kielimu na pongezi kwao na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuondoa changamoto za wanafunzi wa vyuo vikuu huku akitoa mfano wa ongezeko la fedha za kujikimu kutoka kiasi cha shilingi elfu 7 hadi elfu kumi kwa sasa. 

Mpogolo ametumia nafasi hiyo kuwaeleza misingi ya uongozi, utu na nidhamu ili waweze kutimiza malengo yao kwani kiongozi bora ni yule anayeacha alama na uongozi ni historia.

Aidha katika mkutano uwo Mpogolo amewataka viongozi wa tahliso kuimizana kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kujiandikisha na kupiga kura.

Kwa upande wake Rais wa Jumuia ya wanafunzi taasisi za vyuo vikuu Tanzania na kati Zainabu Kitima amesema kikao hiko cha kikatiba kina lengo la kupitia marekebisho ya katiba ya tahliso ambayo iliandikwa miaka 20 iliyopita. 

\Hivyo kufanyika kwa marekebisho hayo kutaifanya jumuia hiyo kufanya kazi kulingana na wakati na mabadiliko ya sekta ya elimu kwa sasa.

Related Posts