Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa alipenda Demokrasia

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kigoma Malima amesema kuwa misingi ya sasa ya Taifa, inayojumuisha uzalendo, umoja na siasa imara ni kutokana na juhudi zilizofanywa na hayati mwalimu Julius kambarage Nyerere za kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa imara na utawala Bora

RC Malima ameeleza hayo kwenye kumbukizi ya hayati mwl Julius kambarege nyerere, ambayo yamefanywa na chuo kikuu cha mzumbe mkoani Morogoro , huku mada kuu ikiwa ni mtazamo wa mwalimu nyerere kuhusu dhana ya uchaguzi huru na haki

Aidha amewataka wananchi pamoja na Viongozi mbalimbali wa kisiasa kuiga mfano wa hayati mwalimu Julius K Nyerere ikiwemo kuyakumbuka mazuri yote aliyoyafanya na wayatumie katika uongozi wao

Naye kwa upande wake Makamo Mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof.William Mwigoha amesema kuwa chuo hicho kimekuwa na taratibu za kumuenzi hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere , ikiwa lengo ni kujadili mitazamo tofauti ya kiongozi huyo hasa katika kusukuma gurudumu la maendeleo , kielimu, uchumi , kisiasa na biashara

Ikumbukwe kuwa hayati mwalimu Julius kambarage nyerere amefikisha miaka 25 tangu afariki dunia Oct 14, 1999, uku chuo cha mzbe kikifanya kumbukizi kwa miaka 21 , ikiwa lengo ni kuifanya jamii hasa vijana kuishi katika misingi imara ya kutambua haki zao na kudumisha amani ya Taifa

 

Related Posts