MENEJA TRA RUVUMA; “KULIPA KODI SIO DHAMBI BALI NI UZALENDO

 Meneja wa TRA mkoa wa Ruvuma Nicodemus Mwakilembe amewataka walipakodi wote kuwa na utaratibu wakulipa kodi kwa hiari na kwawakati kwani kulipa kodi sio dhambi bali ni uzalendo, ili kuepuka adhabu inayotozwa kwani inaweza ikawa kubwa kuliko kodi anayotakiwa kulipa.

Amesema kulipa kodi ni wajibu wa kisheria hivyo ni jukumu la mlipakodi kutekeleza wajibu huu kwa hiari wa kulipa kodi pamoja na  kuwasilisha mawasilisho ya  marejesho ya kodi /tax return, huku akiwakumbusha wauzaji nawanunuzi kutoa nakudai risiti katika kila bidhaa.

Kupitia kilele cha wiki ya huduma kwa wateja Mwakilembe amesema, lengo lakuhitimisha maadhimisho hayo na wateja wao ofisini hapo nikuonyesha namna ambavyo wanawajali wateja kwa kuonyesha utayari wa kuwahudumia nakujenga ushirikianao baina yao na wateja wao hivyo wanaamini kupitia maadhimisho hayo itawasaidia kuvuka lengo la makusanyo ya kodi waliyopangiwa.

Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 walifanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 20 nakusaidia mkoa kuvuka lengo la bilioni 18 walilokuwa wamewekewa, huku akieleza kuwa katika robo hii ya mwaka wa fedha 2024/2025 wamefanikiwa kukusanya karibia  bilioni 7 Sawa na asilimia 108 nakuvuka lengo walilopangiwa.

Ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wateja wote nakuwahimiza kuwa na utaratibu wakutoa nakudai risiti kwani adhabu yakutotoa  risiti ni kuanzia milioni 2 mpaka milioni 4, huku kutodai risiti adhabu yake inaanzia elfu 40 mpaka milioni 1 na nusu.

Akizungumza John Haule kwa niaba ya wafanyabishara waliohudhuria kilele cha wiki ya huduma kwa wateja, amesema wanauhusiano mzuri na TRA kufuatia ukusanyaji wa kodi kwanjia nzuri na rafiki pasipokutumia nguvu ikiwemo kufunga maduka ya wateja yao, huku akitoa rai ya kuendeleza urafiki huo huo kwani wateja wanapenda amani.

Wiki ya huduma kwa wateja Duniani imeadhimishwa kuanzia oktoba 7 nakuhitimishwa leo oktoba 11, ambapo kwa TRA amehitimisha kwa kuwaalika wateja wao ili kuwashukuru kwa ushirikianao wao wanaoutoa katika swala la ulipaji kodi wa hiari.

Related Posts