NHIF KINONDONI YATETA NA WADAU JUMA LA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA


MENEJA Meneja wa ofisi ya NHIF Mkoa wa Kinondoni Dr. Raphael Mallaba amewataka kila mdau atimize wajibu wake ili kufanikisha azma ya pamoja ya kuwapa huduma bora na za viwango vya juu wanachama wa Mfuko.

Tunahitaji kuwa na lugha ya pamoja ili mwanachama ajione wa thamani.

Kila mmoja wetu hapa aone anawajibika kwa mwenzie au kwa lugha ya jumla tunategemeana hivyo tuepuke lugha zisizofaa kwa wanachama tunaowahudumia na kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani kwa sasa Mfuko unachukua hatua stahiki kwa wanaobainika kufanya vitendo hivyo.

Lakini pia aliwataka watoa huduma wawe tayari kuwa mabalozi wa Mfuko sambamba na kuwahudumia watanzania wengi zaidi kutoka ilivyo sasa kwani mwelekeo wa serikali ni utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ambao utaanza kutekelezwa hivi karibuni.

Dr Mallaba aliongeza kwamba Mfuko uko kwenye mageuzi makubwa ya matumizi ya TEHAMA ambapo uboreshaji mkubwa umefanywa kwenye upande wa utambuzi, uhakiki, usajili wa wanachama na uchakataji wa madai, hivyo kutawezesha mwanafunzi vyuo vikuu kujisajili kwa kutumia namba ya udahili (Admission number) na kufanya malipo kwa wakati sambamba na uchakataji na ulipaji wa madai kwa haraka wakati.

Aliyasema hayo wakati akifanya mkutano na wadau wa Mfuko waliopo chini ya Mkoa wa Kinondoni ambao ni waajiri, watoa huduma, wawakilishi wa vyuo vikuu, vyuo vya kati na shule za msingi na sekondari katika kuelekea kilele cha hitimisho la wiki ya huduma kwa mteja lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mfuko huo uliopo kwenye jengo la kibiashara la PSSSF jijini Dar es Salaam leo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau walipongeza uhusiano mzuri uliopo baina yao na Mfuko hususani ofisi ya Mkoa wa Kinondoni lakini pia mrejesho walioupata wa maboresho makubwa yanayotarajiwa na yanayoendelea kutekelezwa kwani wanaona mwelekeo chanya wa Mfuko.

Related Posts