TANESCO SHINYANGA YAHITIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KISHINDO

Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga , Paul Maisori akizungumza wakati wa Hitimisho la maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za TANESCO

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limehitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kukata keki, kunywa chai na wateja wake pamoja na kuwatambua na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi wa Shirika hilo walioonesha umahiri katika kuwahudumia wateja.

Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Ijumaa Oktoba 11,2024 katika ofisi za TANESCO, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga , Paul Maisori amesema wametumia maadhimisho hayo yanayoongozwa na kauli mbiu ‘Ni Zaidi ya Matarajio’ kufurahi pamoja na wateja wao huku akiwashukuru kwa kuendelea kushirikiana na shirika hilo ambalo limeendelea kuboresha huduma zake kila siku.

Katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, TANESCO Mkoa wa Shinyanga imetoa elimu kwa wananchi kuhusu umeme, matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia umeme,

imewatambua wateja wake wakubwa kisha kukata na kula nao keki pamoja na kuwapatia vyeti vya kuwatambua, pongezi na shukrani kwa kulipa ankara za umeme kwa wakati.

Hali kadhalika TANESCO imeendelea kuhamasisha wananchi kulinda miundombinu ya umeme, kutumia huduma ya Nikonekt inayowezesha kuomba huduma ya umeme hata ukiwa nyumbani pamoja na njia mpya ya huduma kwa wateja kupitia Whatsapp iitwayo Jisoti na TANESCO inayorahisisha mawasiliano ya huduma kwa mteja kupitia simu namba 0748550000.

Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga , Paul Maisori akipata chai na wateja wa TANESCO

Related Posts