Wananchi Jitokezeni Kujiandikisha kupiga kura

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Salim ASAS amewasihi wananchi wa mkoa wa Iringa kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha katika vituo vya kujiandikishia kwenye maeneo yao.

ASAS ametoa wito huu leo tarehe 11/10/2024 muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha katika kituo cha afya cha PHC mtaa wa Sabasaba mjini Iringa.

Amesema wananchi wanapaswa kushiriki zoezi hilo kutokana na umuhimu wa uchaguzi huo ambao utawaweka madarakani viongozi wa maeneo yao na viongozi wanaowataka

MNEC amesema kuwa zoezi la kujiandikisha halichukui muda mrefu ambapo yeye ametumia chini ya dakika 2 kukamilisha ambapo amewatolea wito vijana kujitokeza kwa wingi kuandikishwa.

Akizungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika November 27, ASAS amesema anauhakika Chama Cha Mapinduzi CCM kitapata ushindi mkubwa katika mkoa wa Iringa na nchi nzima kutokana na kazi kubwa inayofanywa na serikali katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.

 

Amesema kutokana na ziara alizofanya mkoa mzima wa Iringa ameona wananchi wakiwa na imani na CCM kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao

Hatahivyo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James Amehimiza watu wenye Makampuni au Taasisi mbalimbali kutenga muda pia wa wao kwenda kujiandikisha kupiga kura kwasababu zoezi hilo halitumii mda mrefu

Related Posts