Taasisi ya kibenki ya CRDB imekabidhi mashine ya kuchapishia mitihani katika shule y sekondari Ludewa kwanza Ili kuweza kurahisisha huduma ya utoaji elimu na kuwawezesha wanafunzi kupata mazoezi ya mitihani ya kutosha.
Uwasilishwaji wa mashine hiyo ni matokeo ya maombi ya Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga katika benki hiyo ambapo akiwasilisha changamoto ya shule hiyo na kuwaomba CRDB kuwezesha upatikanaji wa mashine hiyo ambao tayari umetekelezwa.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mbunge Kamonga amelitaka shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilayani Ludewa, kuhakikisha wanawahisha huduma ya umeme kwa wanafunzi wa Shule ya sekondari Ludewa kwanza Ili waweze kusoma vizuri na kutumia vifaa mbalimbali vya umeme kama kopyuta na mashine nyinginezo.
Ameongeza kufuatia changamoto ya uchapishaji mitihani waliyonayo shuleni hapo akaona ni vyema kushirikisha wadau hao Ili waweze kuwasaidia mashine hiyo pamoja na kopyuta hivyo kwa sasa tayari wamewasilisha mashine hivyo vifaa hivyo haviwezi kutumika pasipo umeme.
Hata hivyo kwa upande wake Kaimu meneja TANESCO amesema tayari mchakato upo katika hatua za mwisho ambapo ameahidi kabla ya mwezi huu kuisha umeme utakuwa umewashwa.
Naye Meneja wa CRDB Ndg. Imani amesema benki hiyo inaendelea kutoa michango mbalimbali kwa jamii hivyo katika kuhakikisha kuwa kiwango Cha elimu kinapanda zaidi kunahaja ya kuungwa mkono katika utatuzi wa changamoto.
Shule hiyo ambayo ilianza rasmi kupokea wanafunzi January 2023 imeanza kutoa matokeo mazuri ambapo katika matokeo ya mtihani wa Moko kidato Cha pili mwaka huu kumekuwa na daraja la kwanza na lapili pekee.