Waziri Ridhiwan Kikwete aongoza washiriki zaidi ya 1,000 katika mbio za hisani za kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Ridhiwani Kikwete wameongoza washiriki zaidi ya 1,000 katika mbio za hisani za kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere zilizoanzia eneo la makaburi ya MV. Bukoba Igoma hadi Kisesa Mkoani Mwanza.

Akizungumza na washiriki mara baada ya kuhitimishwa kwa mbio hizo, Kikwete amewapongeza Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza ambao wamebuni mpango huo ambao unaonesha Urithi wa Mwl. Nyerere.

“Baba wa Taifa enzi za uhai wake aliwapigania watanzania kuepukana maadui watatu wa maendeleo ambao ni ujinga, maradhi na umasikini, hivyo leo tunamenzi kwa vitendo kwa mbio hizo zenye kuimarisha afya zetu”

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amebainisha mwitikio mkubwa walioonesha washiriki wa mbio hizo ni ishara kwamba wamehamasika vya kutosha na ushiriki pia wa kilele cha Mwenge wa Uhuru siku ya Oktoba 14, 2024 katila uwanja wa CCM Kirumba.

Related Posts