Aga Khan na wadau wengine wafanya matembezi mahsusi ya kuadhimisha siku ya Afya ya ya akili

Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan Imeungana na Hoteli ya Serena, Dar es Salaam Pamoja aa Lisa Jensen Foundation kuandaa matembezi mahususi ya Afya ya Akili kupitia Mradi wa CHOICE Tanzania

Kama mmoja wa watoa huduma wa afya wakuu nchini, Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan, Tanzania inaendelea kujitolea kwa dhati kukabiliana na changamoto za afya ya akili zinazoongezeka zinazowakabili watu na jamii.

Tamasha hili la kutembea si tu limehusisha jamii bali pia limeimarisha ahadi ya kufikisha ujumbe kua afya ya akili kuwa muhimu sawa na afya ya mwili.

Tamasha hilo liliongozwa na Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Gunini Kamba, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Afya za Aga Khan, Bwana Sisawo Konteh.

Mpango huu ni sehemu ya juhudi kubwa za kuboresha huduma za afya ya akili na ustawi wa maeneo ya kazi, unaoungwa mkono na Shirika la wafanyakazi Duniani (ILO) na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kwa kushirikiana na umma, mpango huu unakamilisha juhudi za Serikali ya Tanzania za kukabiliana na changamoto za afya ya akili na kuimarisha mifumo ya afya katika kanda

Mgeni rasmi, Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Gunini Kamba alisisitiza haja ya kukabiliana haraka na masuala ya afya ya akili, akisema, “Katika miaka ya hivi karibuni, tumeona ongezeko la uelewa kuhusu masuala ya afya ya akili, lakini bado yanakosewa ufahamu na kutozingatiwa, hasa katika maeneo kama yetu. Kama Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, nimeona jinsi hali za afya ya akili zinavyoathiri sio tu watu binafsi, bali pia familia na jamii nzima.

Leo ni mwito wa kuchukua hatua: ni wakati wetu kushughulikia afya ya akili kwa dharura kama afya ya mwili, tukikuza mazingira ya kuunga mkono ambapo kila mtu anajisikia salama kutafuta msaada.”

Akizungumza wakati wa hafla ya tamasha, Bwana Sisawo Konteh, Mkurugenzi Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan, Tanzania alieleza shukrani zake kwa juhudi za pamoja za wadhamini, wadau, na jamii katika kufanikisha tukio hili.

Aliangazia kuwa mipango kama hii inapatikana tu kupitia ushirikiano wa wote waliohusika, akisisitiza mchango muhimu wa wadhamini wakuu kama Hoteli ya Serena, Lisa Jensen Foundation, Benki ya DTB, na New Now Foundation, pamoja na ushirikiano wa washirika mbalimbali wa jamii, ikiwemo Taasisi ya Huduma za Elimu ya Aga Khan na Chuo Kikuu cha Aga Khan.

 

 

Related Posts