RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA SENGEREMA NA MISUNGWI MKOANI MWANZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mama mzazi wa mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) mara baada ya kuwasili Kigongo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Sengerema mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024.

Muonekano wa Daraja la JP. Magufuli linalounganisha eneo la Kigongo (Misungwi) na Busisi (Sengerema) lenye urefu wa km 3 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66. Mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024. Ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 93 na linatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2025.

Shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Sengerema mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024.

Related Posts