Sakata la Mwigizaji Maarufu nchini na familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere lachukua sura mpya

SAKATA LA MWIGIZAJI MAARUFU NCHINI Steve Nyerere na familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere lachukua sura mpya baada ya wazee wa kanda ya ziwa kuingilia kati nakutoa ushauri mzito.
Baadhi ya wazee ambao pia ni wanasiasa wakongwe nchini wakiongozwa na mzee KHAMIS MGEJA wametoa ushauri mzito leo wakiwa katika uwanja wa CCM kirumba katika sherehe ya kuzima Mwenge wa Uhuru.
Baada ya mazungumzo na Steve Nyerere, wazee hao wameshauri pande zote mbili zikae ili wawekane sawa katika mashauri mazuri ambapo Steve Nyerere atapata nafasi nzuri ya utulivu kuwaeleza familia ya Baba wa Taifa kwanini yeye Steve Nyerere aliamua kutumia jina la Baba wa Taifa kama mzazi au mlezi.
Pande mbili hizi zikikutana tunaimani utata ulioibuliwa hivi karibuni na familia ya Baba wa Taifa kupitia Mtoto wake Madaraka utaondoka.
Ikumbukwe, Madaraka Nyerere aliongea na waandishi wa habari akiwa Butiama Mkoa kumkana hadharani Steve kuwa si Mtoto wa Baba wa Taifa na analitumia jina hilo ilihali yeye si mtoto wa Baba wa Taifa na kwamba Steve aache mara moja kutumia jina la Nyerere.
Watanzania wanajiuliza pasipo majawabu endapo Madaraka angelithibitishia Taifa pasipo shaka, muigizaji Steve Nyerere analitumia jina la baba wa Taifa vibaya ikiwemo udanganyifu, ulaghai na utapeli hapo watanzania wangemuelewa vizuri vinginevyo watanzania hawatamuelewa na hawamuelewi kabisa Madaraka
Wazee hao wamesikitishwa sana na maneno ya Madaraka Nyerere na hakupaswa kutoka hadharani. Kwanza wangemuita Steve Nyerere kikaoni nyumbani kumueleza alimaanisha nini kutumia jina la Baba yao.
Wazee hao kwa kauli moja wamemuunga mkono Steve Nyerere na kwamba hakufanya kosa lolote kwa kutumia jina la Nyerere na kwamba kwa kufanya hivyo ameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kulienzi jina la mwasisi wa Taifa na wamewaomba watanzania watambue kuwa Mwl Nyerere ni baba wa Taifa, hivyo watanzania wote ni watoto wa Mwl Nyerere

Related Posts