Serikali yazindua mwongozo wa kusimamia utekelezaji wa miradi ya kimkakati

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Adolf Ndunguru amesema kuwa kuchelewa kukamilika Kwa miradi ya kimkakati Kwa wakati usababisha Serikali isipate thamani halisi ya rasilimali za UMMA nakuzolotesha juhudi za kupunguza umasikini Nchini

Ndunguru ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa mwongozo wa uwanzishwaji na usimamizi wa kampuni Mahsusi za uendeshaji wa miradi ya vitega uchumi kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa(SPV GUIDELINE)

Kutokana na Hali hiyo Ndunguru amesema kuwa hivyo ni muhimu kuwa na usimamizi Bora wa miradi ili kuhakikisha kwamba rasilimali zinazowekwa katika miradi hiyo zinaongezewa thamani na kuleta manufaa makubwa Kwa Watanzania

Aidha Ndunguru amesema kuwa uzinduzi wa Mwongozo huo ni hatua muhimu katika kukabiliana na changamoto hizo Kwa kuweka mazingira salama na endelevu ya uendeshaji na usimamizi wa miradi hiyo ya kimkakati

Mwongozo huo ambao Serikali wanamatumaini makubwa kuwa utakuwa chachu ya mabadiliko katika usimamizi wa miradi ili kuleta Maendeleo ya kiuchumi kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa

 

Related Posts