Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Benki ya CRDB yaja na huduma ya mkopo wa kusaidia usajili kwa wanafunzi wa elimu ya juu usio na riba ili kuwezesha kuhimili gharama za awali kukamilisha usajili wa chuo.
Mkurugenzi wa elimu ya juu toka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msofe amesema mkopo huo utasaidia wanafunzi wenye sifa za kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kukidhi vigezo.
Amefafanua bidhaa hiyo itamuwezesha Mwanafunzi mwenye vigezo vya Kupata Mkopo wa elimu ya juu kulipa gharama za usajili kabla ya Mkopo wake haujamfikia kupitia Mkopo wa Benki ya CRDB unaokwenda Moja kwa Moja chuoni.
“Hii itasaidia kuondoa Malalamiko mengi yanayotolewa na wanafunzi kwamba wanamkopo lakini wanashindwa kujisajili kutokana na kukosa fedha za awali za kukamilisha usajili wao chuoni ili kukidhi vigezo,” alisema Prof. Msofe
Tunawashukuru sana Benki ya CRDB kwa kuona hiyo chagamoto na kuja na bdihaa ambayo itasaidia wanafunzi kupata usajili wao kwa wakati.
Kwa upande wake Meneja kanda ya kati CRDB Chabu Michwaro amesema wao ni wabunifu katika bidhaa zao na huduma kwa wateja na walianza na akaunti ya scholar akaunti mahususi kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu isiyo na gaharama yeyote ile katika kuendesha akaunti na baadae kuja na akaunti ya Boom Advance.