CDF JACOB MKUNDA AWAFIVISHA NISHANI MAJENERALI NA MAAFISA WA JWTZ



MKUU wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Mhe Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Majenerali, Maafisa na Askari wa JWTZ jijini Mwanza tarehe 15 Oktoba 2024.
Nishani hizo ni Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, Nishani ya Miaka 60 ya Muungano pamoja na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.
Aidha,Jenerali Mkunda amewavisha nishani ya Jumuiya ya SADC Maafisa na Askari walioshiriki Ulinzi wa Amani nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa Jumuiya hiyo.

Related Posts