Huduma ya madaktari bingwa wa mama Samia sio sasa :RC Malima

Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima amewataka wananchi kuendelea kuchangamkia fursa za huduma ya madaktari bingwa katika Maeneo Yao maarufu kama Madaktari bingwa wa mama Samia Kwa kupata huduma za bora za matibabu .

Rc Malima ameyasema hayo Mji Morogoro wakati wa kupokea madaktari bingwa 49 ambao wamegawanywa kwenye Halmashauri tisa za mkoa huo ambapo amesisitiza kuwa hilo sio zoezi la kisiasa bali serikali imeamua kurahisisha huduma kwa wananchi hasa vijijini

Malima amesema baadhi ya watu wanaona kuwa ujio wa madaktari bingwa hao kama jambo la kisiasa jambo ambalo halina ukweli wowote bali dhamiria ya Serikali ni nzuri na yenye manufaa Kwa jamii.

“huduma hizi za Kibingwa zinasaidia sana kwani wananchi wangesafiri umbali mrefu kuzifuata lakini huduma hizi zimewafikia hukohuko katika Maeneo Yao”

Madaktari Bingwa hao watatoa huduma ya afya kwa siku sita katika Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro kuanzia Oktoba 14 hadi 20 Mwaka huu.

Mhe. Malima amewasisitiza Madaktari hao kutoa hamasa kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kujua hali za afya zao kwani itasaidia wananchi kujitambua mapema hasa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuanza uchunguzi mapema ili kuanza matibabu mapema.

Kwa upande wake, Mratibu wa Madaktari bingwa wa Rais Samia Mkoa wa Morogoro kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Ismail Mtitu amesema kila Halmashauri za Mkoa huo itapokea madaktari bigwa 6 na muuguzi 1 kuanzia Oktoba 14 hadi 20 Mwaka huu ambao watatoa huduma za kibingwa kwa siku 6.

Sambamba na hayo, Mratibu huyo amesema Madaktari hao wataendelea kusimamia na kusaidia huduma za kibingwa zinatolewa kikamilifu, kuwajengea uwezo Madaktari katika Maeneo husika katika hospitali zilizopo kwenye Halmashauri hizo na kusaidia hospitali kuanzisha wodi maalum za watoto wachanga.

 

 

Related Posts