Waziri Silaa: Tunaendelea kuwekeza kwenye TEHAMA

Na Grace Semfuko, Maelezo

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, amesema Serikali imeendelea kuwekeza kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kufanya maboresho ya kisera, kisheria na kitaasisi pamoja na kujenga uwezo kwa watanzania, lengo likiwa ni kuifanyia Tanzania kuwa sehemu ya mabadiliko ya teknolojia duniani.

Silaa ameyasema hayo leo Oktoba 15, 2024 wakati akifungua kongamano la nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Tanzania, linaloendelea Jijini Dar es Salaam.

Amesema Wizara anayoiongoza pamoja na majukumu mengine, imepewa jukumu la kusimamia sera ya TEHAMA 2016 ambayo inalenga kukuza matumizi ya TEHAMA nchini.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza kwa kasi kubwa katika TEHAMA ambayo ndio nguzo kuu ya kufikia Uchumi wa Kidijitali Duniani, Dunia hivi sasa ipo katika kipindi cha Mapinduzi ya Nne, Tano na Sita ya viwanda ambapo shughuli za kiuchumi, kijamii na uzalishaji kwa kiasi kikubwa inakwenda kuendeshwa kwa kutumia teknolojia za juu za TEHAMA,” amesema Silaa

Related Posts