DC Magoti aahidi kuendeleza na kutunza miundombinu ya unawaji mikono iliyojengwa na Shirika la Water Aid Kisarawe

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Peter Magoti, ameahidi kuendeleza na kutunza miundombinu ya unawaji mikono iliyojengwa na Shirika la Water Aid katika uhamasishaji wa watu kunawa mikono.

Magoti aliyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya kunawa mikono iliyofanyika katika shule ya Msingi Kazumzumbwi Wilayani ya Kisarawe ambapo siku hii huadhimishwa ifikapo Oktoba 15, duniani kote.

Aidha, alisema siku ya kunawa mikono ni muhimu katika kutoa elimu kwa jamii ukizingatia mkono ndio kila kiti na itawaepusha na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya tumbo, macho, kichocho, kipindupindu, kuhara na magonjwa ya homa ya tumbo.

Kampeni ya kunawa mikono iliyoanzishwa na Shirika la Water Aid imefanya pia mambo mengi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya vyoo na kunawa mikono katika shule 30 na vituo 15 vya afya hivyo hawana budi kuvitunza ili viwasaidie kulinda afya za wanamchi na wanafunzi.

Naye Kaimu Mkurugeziwa wa Shirika la WaterAid, Christina Mhando, alisema lengo kuu la mradi wa unawaji mikono ni kuhamasisha tabia siha kwa wananfunzi na watoa huduma za afya walimu na jamii kwa ujumla.

Alisema huwa wanatumia siku hiyo kuwashawishi watunga sera watoa maamuzi, wafadhili na wadau mbalimbali umuhimu wa kuwekeza kwenye maji na usafi wa vyoo na kunawa.

“Tunatoa wito kwa jamii kuona umuhimu wa kunawa mikono kwa jamii kujikinga na magonjwa na kwa watoa huduma kuwakinga wale wanaowahudumia,”alisema

Naye Junita Maiko mwanafunzi wa shule ya Msingi Sungwi alisema katika maadhimisho hayo amejifunza mambo mbalimbali kubwa umuhimu wa unawaji mikono huku akiahidi kwenda kuwa balozi mzuri kwa jamii inayomzunguka.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Sungwi, Shabani Dude, alisema mradi huo umewasaidia hususani katika kuwajengea miundombinu.

Dude aliitaka jamii ielewe kwamba ukipata magonjwa kutokana na kutonawa mikono,wazazi watashindwa kuwalea watoto,watoto watashindwa kupata elimu na kwa ujumla taifa litashindwa kupata maendeleo.

 

Related Posts