Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Sunday Deogratius, amewataka watumishi wote wa serikali wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanajiandikisha kwenye daftari la mpiga kura linaloendelea kote nchini huku akipunguza masaa ya kazi Ili waweze kutimiza adhma hiyo.
Deogratius amesema katika siku hizi za kujiandikisha watumishi wote ambao bado hawajajiandikisha wanapaswa kutoa taarifa kwa wakuu wao wa Idara Ili kuanzia muda wa 8:00 mchana waweze kupewa ruhusa ya kwenda kujiandikisha.
Sanjali na utoaji huo wa ruhusa kwa watumishi lakini pia mkurugenzi huyo akiambatana na mkuu wa Wilaya ya Ludewa Olivanus Thomas wanaendelea na ziara ya kupita kijiji kwa kijiji kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la mpiga kura na kuweza kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika mnamo Novemba 27, mwaka huu.